Idadi ya watumiaji wa WhatsApp Business imeongezeka mara nne katika kipindi cha miaka mitatu
WhatsApp Business ya Meta Platforms' (META.O) sasa inahudumia zaidi ya watumiaji milioni 200 kwenye jukwaa lake, ongezeko ya mara nne kutoka takribani miaka mitatu iliyopita, alisema Mkurugenzi Mkuu Mark Zuckerberg siku ya Jumanne.
Idadi ya watumiaji wa WhatsApp Business imeongezeka mara nne katika kipindi cha miaka mitatu
Biashara ndogo na za kati zitaweza kutuma ujumbe ulioboreshwa kama vile kukumbusha miadi na sasisho kuhusu mauzo ya likizo kwa wateja wao kwa ada. / Photo: AA
28 Juni 2023

Ongezeko hilo la watumiaji linakuja wakati Meta inabadilisha mwelekeo wa maendeleo na ukuzi wa biashara, huku uchumi usio na uhakika ukiathiri biashara kuu ya matangazo ya kampuni hiyo.

Meta ilisema itaanza majaribio kwa vipengele vitakavyosaidia biashara ndogo kuendesha matangazo kwenye jukwaa la ujumbe bila haja ya kuwa na akaunti ya Facebook.

Biashara ndogo na za kati zitaweza kutuma ujumbe ulioboreshwa kama vile kukumbusha miadi na salamu za sikukuu kwa wateja wao kwa bei nafuu.

Meta imekuwa ikifanya kazi ya kutafuta faida kupitia kwa programu zao za ujumbe, WhatsApp na Messenger, kwani Mkurugenzi Mtendaji Zuckerberg anaona ujumbe wa biashara kama kitovu cha kampuni hiyo.

CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us