AFRIKA
2 DK KUSOMA
Uchaguzi wa Zimbabwe: AU-COMESA kuwatuma waangalizi
Zimbabwe inafanya maandalizi ya mwisho ya uchaguzi wake mkuu wa tarehe 23 Agosti 2023. Rais Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kukitetea kiti chake dhidi ya Kiongozi mkuu wa upinzani Nelson Chamisa
Uchaguzi wa Zimbabwe: AU-COMESA kuwatuma waangalizi
Wapiga kura wajiandaa kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa Zimbabwe / Picha: AP
7 Agosti 2023

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, AU Moussa Faki Mahamat, ametangaza kupeleka Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika (AU) na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na Kusini (COMESA) wa Waangalizi wa Uchaguzi (EOM) nchini Zimbabwe.

Ujumbe huo wa pamoja wa AU-COMESA EOM, itawajumuisha waangalizi sabini na watatu (73) wa muda mfupi (STOs) na Timu kuu tatu (3) za wataalam wa uchaguzi, walioratibiwa kuangalia jinsi Uchaguzi huo utakapofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 29 Agosti 2023.

Kulingana na taarifa rasmi kutoka AU, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan akishirikiana na Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda Dk. Ruhakana Rugunda ndio wataongoza ujumbe huo wa pamoja.

Ujumbe huo utashirikiana na wadau mbalimbali na kuangalia maandalizi ya mwisho na mchakato wa upigaji kura na kufanikisha taarifa ya pamoja kuhusu hali ya uchaguzi huo kulingana na utafiti wake punde uchaguzi utakapokamilika.

Madhumuni ya ujumbe huo ni kuhakikisha kuwa chaguzi zinaendeshwa kidemokrasia, uaminifu na amani ili kuchangia uimarishaji wa utawala wa kidemokrasia, amani na utulivu katika taifa hilo.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us