AFRIKA
2 DK KUSOMA
Mahakama ya Gambia yamhukumu mwanajeshi miaka 12 jela kwa jaribio la mapinduzi
Wanajeshi wengine 8 walishtakiwa kwa uhaini na kula njama mwezi Januari kwa jukumu lao katika jaribio la mapinduzi la Desemba 21, 2022.
Mahakama ya Gambia yamhukumu mwanajeshi miaka 12 jela kwa jaribio la mapinduzi
Mshtakiwa , Sanna  Fadera amekana mashtaka yote. Ana siku 30 za kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. / Others
1 Novemba 2023

Mahakama kuu ya Gambia siku ya Jumanne ilimhukumu mwanajeshi Sanna Fadera kifungo cha miaka 12 jela kwa kuongoza mapinduzi yaliyotibuka mwaka jana dhidi ya utawala wa Rais Adama Barrow.

Wanajeshi wengine wanane walishtakiwa kwa uhaini na kula njama mwezi Januari kwa jukumu lao katika jaribio la mapinduzi la Desemba 21, 2022 katika taifa hilo la Afrika Magharibi lenye watu milioni 2.5 inayopakana na Senegal.

Pia raia wengine saba walishtakiwa japo katikati ya kesi, raia hao na wanajeshi saba walioshukiwa kuhusik awaliondolewa mashtaka.

Mwanajeshi anayeshutumiwa kuongoza jaribio hilo l amapinduzi, Sanna Fadera, alipatikana na hatia ya uhaini, mahakama iliamua Jumanne. Askari wengine watatu walioshtakiwa waliachiliwa huru na mashtaka yote.

Fadera amekana mashtaka yote. Ana siku 30 za kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Yamekuwa kitu cha kawaida

Majaribio ya mapinduzi si ajabu kutokea nchini Gambia, ambayo bado inasuasua kutoka kwa zaidi ya miongo miwili chini ya rais wa zamani Yahya Jammeh ambayo iligubikwa na madai ya ubabe na unyanyasaji.

Jammeh mwenyewe alinyakua madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1994 na katika utawala wake amezuia majaribio kadhaa ya kumpindua kabla ya kushindwa katika uchaguzi mwishoni mwa 2016 dhidi ya Barrow.

➤ Fuatilia TRT Afrika Swahili kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika na mashirika ya habari
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us