AFRIKA
2 dk kusoma
Uganda yaipita Ethiopia kwa uuzaji kahawa Afrika
Mauzo ya nje yalikuwa na thamani ya dola za Kimarekani 243,948,952 kwa mwezi wa Mei pekee, hivyo kusukuma jumla ya thamani ya mauzo ya nje kwa mwaka kufikia zaidi ya dola bilioni 2.
Uganda yaipita Ethiopia kwa uuzaji kahawa Afrika
Hawa Nakawungu, mkulima wa kahawa akinyunyizia miti yake dawa ya kuua wadudu kwenye shamba lake karibu na mji mkuu wa Uganda Kampala/ Picha: Reuters .
25 Juni 2025

Mnamo Mei 2025, Uganda iliibuka kama msafirishaji mkuu wa kahawa barani Afrika, ikiweka rekodi ya tani 47,606.7 na kupita mafanikio ya hapo awali ya Ethiopia.

“Mauzo ya nje kwa nchi za Afrika na Asia yalifikia 18% na 13% mtawalia. Mnamo Mei 2025, kiasi cha Uganda kilizidi tani 43,481.02 za Ethiopia, kuashiria mabadiliko makubwa katika mienendo ya biashara ya kahawa barani,” Wizara ya Kilimo ya Uganda imesema katika ripoti yake.

Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa Uganda iliuza mifuko 793,445 ya kilo 60 mwezi uliopita.

Hili ni ongezeko kubwa kutoka mifuko 552,569 mwezi Mei 2024.

Inaashiria ongezeko kubwa la 43.59% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mauzo ya nje yalikuwa na thamani ya dola za Kimarekani 243,948,952 kwa mwezi wa Mei pekee, hivyo kusukuma jumla ya thamani ya mauzo ya nje kwa mwaka kufikia zaidi ya dola bilioni 2.

“Ukuaji wa kipekee katika sekta ya kahawa nchini Uganda kwa kiasi kikubwa unachangiwa na kuimarishwa kwa viwango vya ubora na usaidizi thabiti kutoka kwa Wizara ya Kilimo, Sekta ya Wanyama na Uvuvi,” Wizara hiyo imesema.

Ripoti ya Wizara ya Kilimo imeoneysha kuwa kati ya Juni 2024 na Mei 2025, Uganda iliuza nje magunia 7.43 ya kilo 60 ya kahawa, na kupata dola bilioni 2.09.

Hili ni ongezeko kutoka magunia milioni 6.08 mwaka uliopita.

Italy ilikuwa mnunuzi mkuu kwa 39% ikiwa, Ulaya ilichukua sehemu ya soko ya 67%.


CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us