AFRIKA
4 DK KUSOMA
Rekodi za kushangaza juu ya Mlima Kilimanjaro
Wakati Muingereza Michael Copeland akijiandaa kupanda Mlima Kilimanjaro huku akiwa amebeba friji lenye uzito wa kilo 30 mgongoni, wako waliojiewekea rekodi za kukumbukwa juu ya mlima huo.
Rekodi za kushangaza juu ya Mlima Kilimanjaro
Mwezi Machi mwaka jana, DJ Joozey alikuwa mtu wa kwanza kupiga muziki kwa dakika 15 kwenye kilele cha mlima KIlimanjaro./Picha: Bongo5.com / Others
21 Februari 2024

Kila mwaka, maelfu ya watu hupanda mlima Kilimanjaro, ambao ni mrefu kuliko yote Afrika.

Kati yao, wapo wanaofanya hivyo kama fahari, na wengine huamua kukwea mita 5,895 kama sehemu ya kujiwekea historia muhimu kwenye maisha yao.

Mmoja wao ni DJ Joozey ambaye, mnamo mwezi wa tatu mwaka jana, aliamua kupanda na vifaa vyake hadi kwenye kilele cha Uhuru, na kupiga muziki.

Changamoto tofauti ikiwemo ya hali ya hewa, hususani mgandamizo wa hewa katika maeneo ya mlima huo, hufanya shughuli ya upandaji kuwa pevu zaidi.

Hata hivyo, wapo walioweza kushinda changamoto kama hizo, na kuamua kucheza mpira kwenye mlima huo.

Kati ya wachezaji hao 30 kutoka mataifa zaidi ya 20 duniani pia walikuwepo nyota kama nyota wa zamani wa Marekani Lori Lindsey na mchezaji wa zamani wa Uingereza Rachel Unitt.

Mpiga kinubi huyo aliweka rekodi mpya ya Guinness baada ya kufanya onesho la dakika ishirini, akitumia kinubi chake, kwenye kilele cha juu kabisa barani Afrika .

Hii ilikuwa ni sehemu yake ya kusaidia wale wanaoishi na ugonjwa wa cystic fibrosis.

Cystic fibrosis ni ugonjwa wa kurithi ambao huunda kamasi nene ambazo hunata nata hasa kwenye mapafu na kongosho.

Moja ya sifa ya kuupanda Mlima Kilimanjaro ni utimamu wa kiakili na kimwili. Hata hivyo, Kyle Maynard mtunzi wa vitabu na mtoa hamasa kutoka Marekani alipanda mlima Kilimanjaro kwa 'kutambaa', bila msaada wa vifaa vyoyote.

Mlemavu huyo alitumia siku 10 tu, katika kuweka rekodi hiyo.

Kwa kawaida, upandaji wa Mlima Kilimanjaro, kwa mtu mwenye afya njema, hutumia kuanzia siku tano hadi tisa, kupanda mlima Kilimanjaro, kutegemea na njia itakayotumika.

Anne Lorimor aliithibitishia dunia kuwa umri si kitu chochote bali ni namba tu baada ya kuonesha ujasiri na ushupavu wa kupanda Mlima mrefu kuliko yote Afrika.

Lorimor, kutoka Marekani alitumia njia ya Rongai, mojawapo ya njia za mbali na yenye kufunikwa na msitu.

Pengine hii ndio rekodi ya kushtua na kushangaza zaidi. Wakati waongoza utalii Mlima Kilimanjaro husisitiza neno 'polepole' wakati wote wa kukwea moja ya vilele 7 duniani, mwanariadha Karl Egloff mwenye uaria wa Uswiswi na Ecuador aliamua kukimbia kuelekea kileleni ndani ya saa 4 na dakika 56 tu.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us