MICHEZO
2 DK KUSOMA
Phil Foden ashinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu Ligi Kuu ya Soka Uingereza
Foden mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao 17 na kuwa kutoa pasi za usaidizi nane msimu huu.
Phil Foden ashinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu Ligi Kuu ya Soka Uingereza
Kiungo wa Manchester City, Phil Foden./Picha: Phil Foden X / Others
18 Mei 2024

Kiungo wa Manchester City Phil Foden ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2023/24 wa Ligi Kuu ya Soka ya nchini Uingereza.

"Ninajisikia fahari sana kwa mafanikio haya, " alisema Foden kupitia tovuti rasmi ya Manchester City.

"Ligi Kuu ya Uingereza inafahamika kwa kuwa moja ya ligi bora za duniani na jambo la faraja sana kuchaguliwa kati ya wachezaji wengine wakubwa," aliongeza.

Foden mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao 17 na kuwa kutoa pasi za usaidizi nane msimu huu.

Kiungo huyo pia aliiwezesha Manchester City kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu, mataji matano ya Ligi Kuu ya Uingereza na mawili ya FA.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us