ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Marekani: Bado tunasubiria majibu ya Hamas kuhusu usitishwaji wa mapigano
Vita vya Israeli dhidi ya Gaza vimeingia siku ya 243, vikiwa vimeua Wapalestina 36,550 Palestinians — asilimia 71 wakiwa ni wanawake na watoto wadogo na kujeruhi wengine 82, 959.
Marekani: Bado tunasubiria majibu ya Hamas kuhusu usitishwaji wa mapigano
Kikundi kimoja cha wataalamu kimeonya juu ya uwezekano wa uwepo baa la njaa kaskazini mwa Gaza. / Picha: Reuters   / Others
5 Juni 2024

Jibu kutoka kikundi cha Palestina cha Hamas kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Joe Biden la kusitisha mapigano, bado linasubiriwa mshauri wa masuala ya usalama katika Ikulu ya Marekani, Jake Sullivan amewaambia waandishi wa habari.

"Bado tunangojea jibu kutoka Hamas" kupitia kwa wasuluhishi wa Qatar, Sullivan alisema.

Mkurugenzi wa CIA Bill Burns atakuwa mjini Doha kukutana na wasuluhishi wa Qatar kujadili pendekezo hilo Sullivan aliongeza. Qatar imekuwa msuluhishi kati ya Israeli na Hamas.

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, bado hana utata katika pendekezo la Biden wakati washirika wake wenye msimamo mkali wanachukia makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na Hamas. Wametishia kuvunja serikali ya muungano na Netanyahu ikiwa atakubali mpango huo wa Biden.

Wakati huo huo, msemaji wa Hamas amesisitiza kuwa kikundi hicho hakitokuwa tayari kwa makubaliano yoyote had pale Israeli itakapotoa ahadai ya "wazi" ya mapatano ya kudumu na kujiondoa kabisa kutoka katika eneo la Gaza.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us