ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
'Ni muhimu kumaliza huzuni hii' — Mkuu wa Shirika la Huduma la UN
Mashambulizi ya Israeli dhid ya Gaza yameingia siku ya 247 na kuuwa Wapalestina takribani 36,801, asilimia 71 ikiwa ni wanawake na watoto wadogo na kujeruhi 83,680 huku zaidi ya watu 10,000 wakiwa wamefunikwa na vifusi.
'Ni muhimu kumaliza huzuni hii' — Mkuu wa Shirika la Huduma la UN
Mkuu wa Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa amesema hakuna Gaza si sehemu salama tena / Picha: AA / Others
9 Juni 2024

Mkuu wa shirika la misaada ya Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu shambulio la Israeli dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza na kusababisha vifo vya watu 210 na wengine zaidi ya 400 kujeruhiwa.

"Leo hii, kambi ya wakimbizi ya Nuseirat ndio kitovu cha kiwewe cha matatizo ya watu wa Gaza.

Picha za vifo na uharibifu kufuatia operesheni ya kijeshi ya Israeli zinathibitisha kwamba kila siku vita hivi vinaendelea, vinazidi kuwa vya kutisha," Martin Griffiths alisema katika taarifa yake.

Griffiths alisisitiza kuwa hakuna mahali salama huko Gaza na huduma ya afya katika eneo lililozingirwa.

"Na hata wakati mateka wanne wanaunganishwa tena na familia zao, tunakumbushwa kwamba bado watu wengi wanashikiliwa. Wote lazima waachiliwe. Raia wote lazima walindwe. Huzuni hii ya pamoja inawezekana na ni lazima iishe ," aliongeza.

Pata Habari Zaidi kupitia WhatsApp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us