AFRIKA
2 DK KUSOMA
Uganda yapiga marufuku 'disko matanga'
Kulingana na serikali ya nchi hiyo, shughuli hizo husababisha kuporomoka kwa maadili.
Uganda yapiga marufuku 'disko matanga'
 Waziri wa Uganda Justine Kasule Lumumba amesema kuwa shughuli hizo zimepigwa marufuku mara moja. / Picha: Justine Kasule Lumumba   / Others
8 Oktoba 2024

Serikali ya nchini Uganda imepiga marufuku "disko matanga" huku ikisisitiza kuwa shughuli hizo zinachochea unyanyasaji wa kijinsia.

Miziki hiyo, ambayo huchezwa nyakati za usiku, huhusisha wanawake ambao huwapa burudani wanaume ili wapate pesa kwa ajili ya shughuli za mazishi.

Hata hivyo, shughuli hizo, zimepigwa marufuku na asasi za haki za kiraia kwa kusababisha unyanyasaji wa kingono.

"Hizi ni shughuli za kishetani, na wale watakaopatikana wakiendeleza vitendo hivi, watachukuliwa hatua kali za kisheria," alisema Waziri Justine Kasule Lumumba katika mahojiano yake na AFP.

'Asili yake Kenya'

"Wasichana wadogo hucheza majukwaani huku wamevaa nusu uchi ila kuwavutia wanaume waweze kuchangia kwenye shughuli za mazishi," alisema.

Kulingana na Waziri huyo, shughuli hiyo iliyoasisiwa nchini Kenya, inazidi kupata umaarufu, hasa katika maeneo ya Mashariki mwa Uganda.

Kenya yenyewe ilipiga marufuku miziki hiyo, mwaka 2018.

Afisa mmoja kutoka wilaya ya Namayigo iliyoko mashariki mwa Uganda, Suleiman Walugembe Juuko, aliiambia AFP kuwa miziki hiyo pia huhusisha ulevi na matumizi ya dawa za kulevya, ambayo huchochea vurugu.

'Kusimamia marufuku hiyo'

"Tuna matukio mawili ya watu kupoteza maisha kutokana na disko matanga, msichana mmoja alibakwa wakati kijana mwingine aliuwawa wakati anatoka kwenye disko matanga," Juuko alisema.

"Tunatekeleza katazo hili," aliongeza.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika na mashirika ya habari
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us