AFRIKA
2 DK KUSOMA
Profesa Janabi kuchukua nafasi ya Dkt Ndugulile WHO?
Profesa Mohamed Janabi atawania nafasi ya mkuu wa WHO kwa kanda ya Afrika kufuatia kifo cha Dkt Faustine Ndugulile kilichotokea Novemba 27.
Profesa Janabi kuchukua nafasi ya Dkt Ndugulile WHO?
Profesa Mohamed Janabi./Picha: Wengine / Others
10 Desemba 2024

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemtangaza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Profesa Mohamed Janabi kugombea nafasi ya ukuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kanda ya Afrika.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Samia amesema kuwa ana imani na uzoefu wa mtaalamu huyo wa afya nchini Tanzania.

“Ngoja niwape siri siku ya leo. Tumepitia sifa za wenzako watano na tukaona kuwa kuwa jina lako linafaa kupelekwa WHO kw ajili ya kushindania nafasi hiyo. Kwahiyo tunajiandaa kwa hilo na wakati ukifika, tutapeleka jina lako WHO, na ni vizuri ukajiweka tayari kuanzia sasa,” alisema Rais Samia wakati akiwaapisha viongozi hao katika ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

Iwapo atachaguliwa, Profesa Janabi atachukua nafasi ya Faustine Ndugulile aliyefariki dunia nchini India wakati akipatiwa matibabu.

Kwa sasa, Profesa Janabi ambaye amejizolea umaarufu nchini Tanzania kutoka na mafunzo yake ya lishe bora, ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, akiwa pia ameteuliwa kuwa mshauri wa Rais wa masuala ya afya.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us