UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki inasherehekea siku ya Uhuru na Siku ya Watoto, ikiwa pia ni siku ya kuanzishwa kwa Bunge
Huku sauti za watoto zikirindima kote nchini, Uturuki inaadhimisha kuanzishwa kwa bunge pia, ambapo mbegu ya uhuru ilipandwa na kutoa fursa kwa vizazi vya baadaye.
Uturuki inasherehekea siku ya Uhuru na Siku ya Watoto, ikiwa pia ni siku ya kuanzishwa kwa Bunge
23 Aprili 2025


Uturuki inasherehekea siku ya Uhuru wa Taifa na Siku ya Watoto, ikiadhimisha miaka 105 tangu kuanzishwa kwa bunge la Kitaifa mwaka 1920, msingi muhimu katika historia ya sasa ya nchi hiyo.

Siku hii, ambayo pia inasisitiza umuhimu wa watoto kama viongozi wa baadaye, ilisherehekewa na hafla rasmi, maonesho ya kitamaduni, na watu kukusanyika wakifurahi kote nchini.

Sikukuu hii ya kitaifa, ni ya kipekee duniani kwa kuwa inaunganisha demokrasia ya bunge na haki za watoto, ni moja ya siku muhimu katika sherehe za Uturuki. Shule zilikuwa na hafla maalum zilizojumuisha nyimbo, kucheza, na kughani mashairi, huku watoto wakikaa kwenye mfano wa viti bungeni na wizara ikiwa ni utamaduni wa muda mrefu wa kuimarisha elimu ya siasa na kushirikisha watoto katika masuala ya nchi.

Bunge la Taifa la Uturuki, lilianzishwa Aprili 23, 1920, jijini Ankara, na kuanza kwa harakati za kupata uhuru kamili. Uamuzi wa Ataturk wa kutenga siku hii kwa watoto mwaka 1929 ulikuwa wa msingi sana ambao umekuwa ishara ya dhamira ya Uturuki kwa vijana wake.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us