AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Ruto asaini mikataba 7 na Uchina ya uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 823
Sekta ya kibinafsi ya Uchina imekuwa muhimu katika kukuza ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa miaka mingi kupitia uwekezaji wao katika sekta mbalimbali za uchumi wetu- Ruto
Rais Ruto asaini mikataba 7 na Uchina ya uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 823
Rais Ruto alitoa wito kwa Kenya na China kuendelea kupigania lengo la Global South katika mikutano ya kimataifa, hasa haja ya kufanya mageuzi ya taasisi za kimataifa ili kuwa na uwakilishi zaidi na ufanisi. / Others
23 Aprili 2025

Kenya na Uchina wamesaini mikataba mipya 7 ya thamani ya zaidi ya dola 823 za Marekani.

Mikataba hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inahusisha sekta ya kibinafsi ya Uchina, inatarajiwa kuleta ajira kw amaelfu ya vijana kupitia ewekezaji hasa katika sekta za Ushafirishaji na ujenzi.

‘‘Tunajitahidi kuhimiza ushiriki mkubwa zaidi wa sekta ya kibinafsi ya China katika safari yetu ya mageuzi ya kiuchumi, ambayo kwa upande wake, itaunda maelfu ya ajira kwa vijana wetu,’’ alisema Rais Ruto.

Rais William Ruto anafanya ziara ya siku nne nchini Uchina kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais Xi Jinping.

Vita vya kiuchumi

‘‘Tunatafuta kukuza na kupanua uhusiano wa kihistoria, kiuchumi na kitamaduni ambao umefafanua uhusiano mzuri kati ya Kenya na Uchina kwa miaka mingi,’’ alisema Rais Ruto.

Wakati huo huo, Rais William Ruto alisisitiza hitaji la dharura la kuunda mpangilio mpya wa ulimwengu, ambao unazingatia hali halisi ya kiuchumi ya sasa.

Ruto alikuwa aliyasema haya wakati wa mhadhara wa umma katika Chuo Kikuu cha Peking huko Beijing uliohudhuriwa na wadau wa biashara kutoka sekta za kibinafsi na serikali.

‘‘Usanifu wa kifedha na usalama ulioibuka kutokana na mzozo huo umefaidi kwa kiasi kikubwa Global North kwa gharama ya Global South bila kujumuisha kila mtu mwingine,’ alisema.

TRT Global - Rais Ruto kuongoza kongamano la biashara nchini China

Ni katika ziara yake ya kiserikali ya siku nne nchini humo, ambapo mbali na hiyo, pia atajadiliana masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na mwenyeji wake Xi Jinping.

🔗

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us