Uturuki imepongeza uamuzi wa Marekani wa kuiondolea vikwazo Syria, “wakiuita hatua chanya.”
Katika taarifa yake ya Jumanne kwenye ukurasa wake wa X, Ankara ilipongeza uamuzi huo wa kusawazisha mahusiano na serikali ya Syria, alisema Oncu Keceli, msemaji wa Wizara hiyo siku ya Jumanne.
Uturuki itaendelea kuchangia kwenye ujenzi mpya wa Uturuki, haswa katika sekta ya umma na ile ya binafsi, kwa kushirikiana na wadau wa kikanda na wa kimataifa,” aliongeza.
Kauli hiyo ya Uturuki inakuja baada ya serikali ya Donald Trump kuonesha nia hiyo.
"Marekani iko tayari kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinatawala nchini Syria na kwa majirani zake pia," alisema Trump katika amri yake iliyowekwa kwenye ukurasa wa X.
'Hatua muhimu'
Kwa upande wake, Syria ilipongeza hatua hiyo, ikisema kuwa itatoa fursa ya ujenzi mpya wa nchi hiyo na kuhuisha utangamano wake ndani ya jumuiya ya kimataifa.
“Tunapongeza uamuzi wa kuondoa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria uliotiwa saini na Rais Trump,” alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al Shaibani kupitia ukurasa wa X.
Aliuelezea uamuzi huo kama hatua muhimu ambayo itaiwezesha Syria kupata ustawi na utulivu.
“Milango ya ujenzi mpya iko wazi baada ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo,” alisema Shaibani akiongeza kuwa uamuzi huo utasaidia ukarabati wa miundombinu muhimu nchini humo na kusaidia Wasyria kurejea kwao.