AFRIKA
2 dk kusoma
"Mnasema 'Ruto must go,' niende vipi?" Auliza Rais wa Kenya
Rais William Ruto amewakashifu waliaondamana 25 Juni kwa kutaka aondoke madarakani akisema kuwa katiba ya Kenya ina muongozo wa mihula ya uongozi.
"Mnasema 'Ruto must go,' niende vipi?" Auliza Rais wa Kenya
Rais wa Kenya William Ruto amekashifu uahribifu wa biashara na mali wakati wa maandamano 25 Juni 2025/ Picha: William Ruto / Public domain
27 Juni 2025

Rais wa Kenya William Ruto amewakashifu walioandamana 25 Juni 2025 katika sehemu tofauti nchini akidai kuwa hawana muongo wa suluhisho.

“Nimewasikiliza wanaoandaa maandamano na nimeelewa mambo matatu hivi. Kwanza wanaipenda Kenya lakini hawataki viongozi. Pia wamesema mambo ya muhulu mmoja wa uongozi,”Rais Ruto alisema akiwa katika mkutano na wajasiriamali wadogo wadogo jijini Nairobi.

Maandamano yaliadhimisha mwaka mmoja tangu ya Juni 2024 yaliyopinga muswada wa fedha 2024. Pia yalipinga ukatili wa polisi.

Serikali imesema kuwa zaidi ya watu kumi waliuawa katika maandamno hayo huku zaidi ya 400 wakijeruhiwa wakiwemo maafisa wa polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen alikashifu uharibifu wa mali, baadhi ya vituo vya polisi kuchomwa.

“Kwa hivyo nawauliza hivi kama unapenda Kenya unavyosema usichome nchi yako, kama unatuambia unapenda nchi hii usiwe sehemu ya matatizo yake, angalia jinsi ya kupata suluhisho,” Rais Ruto amesema.

Amedai kuwa maandamano yanafanywa kwa msingi wa chuki.

“Ikiwa unawachukia viongozi, chuki huleta mzozo, mzozo huleta vita, vita sio suluhisho kwa ukosaji wa ajira au changamoto zozote za Kenya. Kama mikakati yako yana msingi wa chuki kwa wengine na kwa viongozi je, utapata suluhu kwa nchi yetu? ” Rais huyo ameuliza.

Ameonya kuwa maandamano yakiendelea kuwa ya uharibifu yataharibu biashara ya ngazi tofauti.

Muhula wa Uongozi

Kati ya kauli mbiu ambazo waandamanaji walitumia 25 Juni ni “wantam” ikiashiria kuwa Rais Ruto anafaa kuongoza muhula mmoja tu .

Katiba ya Kenya inaruhusu rais kuwania muhula wa pili wa miaka mitano kupitia uchaguzi.

“Kama ni suala la muhulu wa uongozi, katiba imefafanua, unaweza kuwa na muhula mmoja au mbili hakuna zaidi katiba inasema wazi. Tafadhali tutafute suluhisho ambalo haijajikita kwa muhula wa ungozi ila kwa mipango ya maendeleo.”

Pia amekashifu kauli mbiu ya “Ruto must go” ( Ruto lazima aondoke) ambayo waandamanaji walitumia Juni 25 lakini pia imekuwa ikitumika sana mitandaoni na katika mikutano ya wananchi.

“Tuwe wa kweli munamaanisha nini na “ Ruto must go,” niende vipi kwa sababu tuna katiba. Ikiwa unataka Ruto aende ushauri wangu ni ‘pata maono bora zaidi na uwashawishi Wakenya’“

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us