UTURUKI
3 dk kusoma
Uturuki inapongeza mpango wa Israel na Iran, inalaani mashambulizi ya Israel huko Gaza: Erdogan
Rais wa Uturuki amesema kuwa Ankara inaunga mkono jitihada za upatanishi za Donald Trump.
Uturuki inapongeza mpango wa Israel na Iran, inalaani mashambulizi ya Israel huko Gaza: Erdogan
Rais huyo wa Uturuki alilaani vikali mashambulizi ya Israel yanayoendelea gaza, akionya juu ya uwezekano wa kutokea kwa janga la kibinadamu./Picha: AA
25 Juni 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa nchi yake inaunga mkono mpango wa usitishwaji mapigano kati ya Iran na Israel, akiongeza kuwa anategemea pande zote hizo “kukubaliana na wito wa rafiki yangu (Rais wa Marekani) bila masharti yoyote”.

Katika risala yake baada ya mkutano wa NATO jijini The Hague siku ya Jumatano, Erdogan alithibitisha kuwa Uturuki imehusishwa na jitihada za kidiplomasia zinazohusu mzozo kati ya Israel na Iran, akiongeza kuwa “zinahatarisha usalama wa kanda”.

Alisisitizia imani ya Ankara kuwa “amani ya kudumu na Iran itapatikana kupitia diplomasia na mazungumzo”, akisema “kanda yetu imejaa mizozo ambayo uharibifu wake hautotupeleka popote”.

Erdogan alisema kuwa Uturuki ina imani kuwa “uamuzi huo utaleta utulivu wa kudumu”, akisema kuwa “kila mtu ana jukumu la upatikanaji wa amani ya Mashariki ya Kati”.

Gaza hatarini kuingia kwenye ‘janga la kibinadamu’

Rais huyo wa Uturuki alilaani vikali mashambulizi ya Israel yanayoendelea gaza, akionya juu ya uwezekano wa kutokea kwa janga la kibinadamu.

“Kwa miaka mitatu mfululizo, Wapalestina wameendelea kuwa shabaha,” alisema Erdogan. Kulingana na Erdogan, mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watu 56,000, “wengi wakiwa ni wanawake na watoto”, na kuongeza kuwa “asilimia 80 ya Gaza, imeharibiwa”.

Erdogan alisema kuwa kwa makusudi kabisa, serikali ya Israel ilikuwa ikizuia misaada ya kibinadamu kuingia katika maeneo yaliyozingirwa.

Akitoa wito kwa jumuiya za kimataifa, Rais wa Uturuki alisema: “Mtu yeyote mwenye dhamiri hawezi kulikalia kimya suala hili. Ningependa kutoa wito kwa kila mtu mwenye kujali uhai wa binadamu kupaza sauti zao dhidi ya unyanyasaji huu.”

Pia alionya kuwa vitendo vya Israel vilikuwa vikihatarisha sio tu usalama wa Gaza, bali eneo zima la Mashariki ua Kati. "Israel inahatarisha usalama wa kanda na kwa kufanya hivyo, wanakandamiza usalama wa watu wake," alisema Erdogan.

“Kama nchi nyingine katika ukanda huu, usalama wa Israel unategemea amani, utulivu na ustawi wa majirani zake. Mashambulizi ya Israel yamefanya hali ya kibinadamu ya Gaza kuwa janga ambalo halipaswi kufumbiwa macho na mtu yeyote yule mwenye dhamira.”

Jitahada za kuondoka vikwazo kwenye biashara ya ulinzi

Kuhusu mtangamano wa ulinzi, Rais huyo wa Uturuki alisema kuwa alisisitizia ushirikishwaji wa nchi zisizo wanachama wa Umoja wa Ulaya “ni kwa maslahi ya Ulaya nzima”.

Hali kadhalika, Ankara inaendesha mazungumzo na London na Berlin kuhusu mpango wa ndege vita za Eurofighter, akiongeza kuwa “kuna maendeleo chanya”.

 Vile vile, alipongeza hatua ya hivi karibuni na mshirika wake Marekani: “Tumejadiliana suala la ndege vita za F-35. Tumefanya malipo ya kati ya dola bilioni 1.3 hadi dola bilioni 1.4 kwa ajili ndege hizo, na tunaona nia njema ya Trump ya kufanikisha mpango huo.”

Kwa upande mwingine, Erdogan alisema kuwa Uturuki ilikuwa ikiongoza jitihada za kuhakikisha kuwa “NATO inaondoa vikwazo vyote vya biashara ya kiulinzi”.

“Pia, tumehakikisha kuwa azimio hilo linaakisi mawazo yetu kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yatafanikiwa tu kupitia mshikamano,” alisema.

CHANZO:TRT World and Agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us