UTURUKI
1 dk kusoma
Umoja wa Afrika, Uturuki waipongeza Somalia kwa kuadhimisha miaka 65 ya uhuru
Somalia ilipata uhuru wake mwaka 1960 baada ya miaka mingi ya utawala wa kikoloni.
Umoja wa Afrika, Uturuki waipongeza Somalia kwa kuadhimisha miaka 65 ya uhuru
Somalia inaadhimisha Siku yake ya 65 ya Uhuru mnamo Julai 1. / AA
1 Julai 2025

Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), Jumanne ilitoa "pongezi za dhati" kwa serikali na watu wa Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia kwa kuadhimisha miaka 65 ya uhuru wa nchi hiyo. Somalia inaadhimisha Siku yake ya Uhuru mnamo Julai 1.

Mwenyekiti wa AUC, Mahmoud Ali Youssouf, aliangazia umuhimu wa kihistoria wa siku hiyo, akibainisha kwamba Julai 1, 1960, iliashiria uthibitisho wa umoja, uthabiti, na azma ya watu wa Somalia.

"Mnapoadhimisha hatua hii muhimu, natoa pongezi kwa vizazi vya Wasomali ambao kujitolea kwao kumefanikisha siku hii," Youssouf alisema katika taarifa ya pongezi.

AUC ilisema safari ya Somalia tangu uhuru ni safari "iliyoangaziwa na ujasiri, uvumilivu, na kujitolea kujenga Somalia yenye amani, demokrasia na ustawi."

Uturuki inaipongeza Somalia

Uturuki pia iliipongeza Somalia kwa kuadhimisha miaka 65 ya uhuru, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ikisifu uhusiano wa "kirafiki na kindugu" kati ya nchi hizo mbili.

"Hongera kwa Somalia nchi yenye kirafiki na undugu katika Siku yake ya Kitaifa," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki iliandika kwenye mtandao wa X.

Uhuru wa Somalia tarehe 1 Julai 1960, ulitokana na kuunganishwa kwa maeneo mawili tofauti ya kikoloni - yaliyokuwa yakitawaliwa na Uingereza na Italia.

InayohusianaTRT Global - Uturuki, Somalia wasaini makubaliano ya uchimbaji gesi ya ‘haidrokaboni’ baharini
CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us