AFRIKA
1 dk kusoma
Umeme wakatika Sudan baada ya shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani katika kituo kimoja
Shambulizi hilo ni la hivi karibuni la ndege zisizokuwa na rubani katika miundombinu ya umeme kaskazini mwa Sudan ambapo mamlaka zimekuwa zikilaumu wapiganaji wa RSF.
Umeme wakatika Sudan baada ya shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani katika kituo kimoja
Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakilaumiwa kwa mashambulizi katika miundombinu ya umeme. / Reuters
25 Aprili 2025

Shambulio la ndege isiyokuwa na rubani siku ya Ijumaa lililenga kituo cha umeme cha Atbara kaskazini mwa Sudan, na kusababisha umeme kukatika katika majimbo ya Mto Nile na Bahari ya Shamu pamoja na kuwepo kwa moto mkubwa, hii ni kulingana na shirika la umeme la Sudan.

“Kituo cha umeme cha Atbara kilishambuliwa leo na ndege isiyokuwa na rubani, na kusababisha kukatika kwa umeme katika majimbo ya Mto Nile na Bahari ya Shamu,” shirika la Umeme la Sudan lilisema katika taarifa.

Maafisa wa kukabiliana na dharura walikuwa wanajitahidi kuzima moto, na mafundi walikuwa wanatathmini hasara kwanza kabla ya kuanza ukarabati, iliongeza.

Shambulizi hilo ni la hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulio ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani kwa miundombinu ya umeme kaskazini mwa Sudan. Mashambulizi mengine katika siku za karibuni yamelenga maeneo muhimu ya umeme kama Merowe, Dongola, Al-Dabba, na Atbara.

Mamlaka nchini Sudan zimekuwa zikilaumu wapiganaji wa RSF kwa kufanya mashambulizi hayo, ingawa kundi hilo halijasema chochote kuhusu matukio haya ya sasa.

Mapigano kati ya vikosi vya RSF na jeshi yalianza 15 Aprili, 2023 na tangu wakati huo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu na moja ya hali mbaya zaidi kwa watu duniani.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us