Kanisa la Kipentekoste nchini Afrika Kusini lilisherehekea Jumapili ya Pasaka kwa sherehe kubwa za harusi kwa takriban watu 3,000 kwa mara moja, huku wengi wao wakiingia kwenye ndoa za wake wengi.
Kanisa la International Pentecost Holiness Church lilisema harusi za umati ni sehemu ya sherehe zake za Pasaka na utamaduni wa wake zaidi ya mmoja.
Sherehe za Jumapili zingeshuhudia baadhi ya wanaume wakioa wake zao wa sita au wa saba, msemaji wa kanisa Vusi Ndala alisema. Maharusi wengine walikuwa wamepangwa kuoa wachumba wengi kwa wakati mmoja, Ndala alisema.
"Ndoa za wake wengi sio tu kukubalika tu bali pia kuheshimiwa sana" kanisani, Ndala alisema.
Harusi ya mwaka huu ni kubwa zaidi
Kanisa la International Pentecost Holiness Church lilianzishwa nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa miaka ya 1960.
Kanisa hilo liliwahi kufanya harusi kubwa hapo awali, ikiwa ni pamoja na mwaka wa 2023 ambapo karibu wanandoa 400 au karamu za harusi zilifunga ndoa. Inasema tukio la mwaka huu lilikuwa kubwa zaidi kwa mbali.
Ndala alisema idadi kubwa ya watu wanaooa mwaka huu ni kwa sababu ya "idadi kubwa ya wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja."
Katika visa fulani, wachumba walileta mke au wake zao wa sasa ili wawe pamoja nao kwa ajili ya ndoa yao mpya.
Kuoa wake wengi inaruhsuiwa kimila
Harusi hizo zilifanyika katika makao makuu ya kanisa hilo, jengo kubwa lenye umbo la kuba katika mji wa Heidelberg, karibu na Johannesburg, ambalo linaweza kuchukua watu 60,000.
Washirika ambao walikuwa wamefunga ndoa walisubiri katika mahema marefu meupe yaliyowekwa kwenye uwanja wazi karibu na jengo la kanisa, ambapo walipewa maua ya arusi, pakiti za chakula na maji.
Kisha wakaingia ndani ya jengo la kanisa kwa foleni ndefu, wanawake wakiwa wamevalia gauni nyeupe za harusi na wanaume wengi waliovalia suti nyeupe na tai nyekundu zinazofanana.
Kuoa wake wengi ni halali nchini Afrika Kusini ikiwa muungano huo umesajiliwa kama ndoa ya kimila.