MICHEZO
2 dk kusoma
Liverpool 'kufunga kazi' Jumapili?
Liverpool imebakisha mechi tano katika Ligi Kuu ya England msimu huu lakini inahitaji alama moja pekee kuchukua ubingwa.
Liverpool 'kufunga kazi' Jumapili?
Liverpool ilikuwa karibu kuchukua ubingwa siku ya Jumatano. /Reuters
25 Aprili 2025

Kocha wa Liverpool Arne Slot anaamini Liverpool wana "jukumu kubwa" katika kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England mbele ya mashabiki wao watakapokabiliana na Tottenham Jumapili katika uwanja wa Anfield.

Vijana wa Slot watatangazwa kuwa mabingwa kwa mara ya 20 kama watafanikiwa kuepuka kushindwa na Tottenham.

Liverpool imebakisha mechi ya tano na inahitaji alama moja tu ili ichukue ubingwa.

Ushindi wa Liverpool miaka mitano iliopita haukuwa na mbwebwe nyingi, kwa sababu ulitokea wakati wa janga la Covid-19, kumaanisha uwanja wa Anfield ulikuwa hauna watu wakati wa kukabidhiwa taji kutokana na masharti ya kutotoka nje.

Shinikizo

Na baada ya mechi ya Jumapili na Tottenham, Liverpool inakwenda London kukabiliana na Chelsea, Slot anakiri kuwa kuna shinikizo zaidi la kumaliza kazi katika uwanja wa nyumbani.

"Ni jukumu kubwa kwetu sisi. Tunafahamu kuwa mara ya mwisho klabu hii kushinda ilikuwa kipindi cha Covid. Kwa hiyo tunajiandaa sana kwa Jumapili," Slot aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa.

"Tunafahamu bado kuna kazi ya kufanya. Tunahitaji japo alama moja. Mashabiki wetu wanafahamu hilo pia. Wanapokuja uwanjani, lazima watushabikie kwa njia nzuri zaidi, kama walivyofanya msimu mzima.

"Ni mechi nzuri ukizingatia lakini pia ni jukumu kubwa kwetu siku ya Jumapili."

Ushindi ulikuwa karibu

Karibu Liverpool ipate ushindi siku ya Jumatano wakati Arsenal ilipopata sare ya 2-2 na Crystal Palace, ambapo vijana wa Slot wangechukua ubingwa iwapo Crystal Palace wangeifunga Arsenal katika uwanja wa Emirates.

Slot na wachezaji wake walikusanyika pamoja kutizama mechi ya Arsenal wakiwa na matumaini ya kusherehekea.

Sasa Liverpool imeizidi Arsenal na alama 12, ambapo Arsenal imebakisha mechi nne, kwa maana hiyo timu hiyo itabidi ipambane dhidi ya Tottenham ili kuwafurahisha mashabiki wake wa nyumbani.

"Ilikuwa tofauti. Kwa kawaida ukitizama mechi ya soka, uko peke yako au na familia au marafiki. Lakini wakati huu tulitizama pamoja," Slot alisema.

"Kabla ya mechi hiyo, ningeshangaa kama mchezo ungemalizika kwa sare. Lakini wakati wa mechi, sikushangaa kwa sababu Crystal Palace ilionesha kile ambacho ligi hii inataka."

- 'Klabu hii lazima ishinde mataji' - Tuwe sawa na mahasimu wetu Manchester United tukiwa na makombe 20 na itakuwa tumewafurahisha zaidi mashabiki wa Liverpool.

Na akiwa katika msimu wake wa kwanza tangu kumrithi Jurgen Klopp, kocha huyo wa zamani wa Feyenoord Slot atakuwa kocha wa 12 kushinda Ligi Kuu ya England na Mholanzi wa kwanza kufanya hivyo.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us