AFRIKA
3 dk kusoma
Nigeria yaondoa mswada unaotaka wasiopiga kura kufungwa hadi miezi sita
Bunge la Kitaifa la Nigeria limetupilia mbali mswada ambao ungefanya upigaji kura kuwa wa lazima, taarifa kutoka kwa spika wa Baraza la Wawakilishi alisema Jumatatu.
Nigeria yaondoa mswada unaotaka wasiopiga kura kufungwa hadi miezi sita
Idadi ya wapiga kura nchini Nigeria kwa miaka mingi imepungua. / Picha: AFP
27 Mei 2025

Bunge la Kitaifa la Nigeria limetupilia mbali mswada ambao ungefanya upigaji kura kuwa wa lazima, taarifa kutoka kwa spika wa Baraza la Wawakilishi ilisema Jumatatu kufuatia upinzani kutoka kwa wanasheria na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Mswada huo - ambao ulipendekeza kifungo cha miezi sita jela au faini ya naira 100,000 kwa wapiga kura wanaostahiki ambao walishindwa kupiga kura, ulisomwa kwa mara ya pili bungeni - siku 10 zilizopita.

Taarifa kutoka kwa afisi ya spika Abbas Tajudeen, ambaye alifadhili mswada huo, ilisema ameamua kuuondoa mswada huo "kufuatia mashauriano ya kina na wigo mpana wa washikadau."

Mswada huo "uliwasilishwa kwa nia nzuri zaidi, ambayo ni kuimarisha ushirikiano wa raia na kuimarisha demokrasia yetu kwa kuhimiza idadi kubwa ya wapiga kura," ilisema taarifa hiyo.

Ushiriki umepungua kwa miaka

Idadi ya waliojitokeza katika chaguzi za kitaifa nchini Nigeria imepungua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, huku uchaguzi wa urais wa 2023 ukirekodi idadi ya waliojitokeza kupiga kura kwa asilimia 27, idadi ndogo zaidi tangu taifa hilo kurejea katika utawala wa kidemokrasia mwaka 1999.

Aliyekuwa Gavana wa Lagos, Bola Tinubu alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 37 ya kura zilizopigwa katika mojawapo ya chaguzi zilizokuwa na vita vikali nchini Nigeria.

"Upigaji kura wa lazima kwa muda mrefu umekuwa ukifanyika kwa mafanikio makubwa katika nchi kama vile Australia, Ubelgiji na Brazil," taarifa ya spika ilisema.

Lakini mashirika ya haki za Nigeria yalipuuzilia mbali jaribio hilo, huku baadhi wakiitaja kuwa ni la kibabe na ni kinyume cha katiba.

'Haiendelezwi kwa kulazimishwa'

Shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu Abuja, ambalo linakuza utawala wa kidemokrasia, haki za binadamu na ushirikishwaji wa raia lilisema muswada huo "ni wa kibabe na unajumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za kimsingi zinazohakikishwa na kikatiba."

Demokrasia haiendelezwi kwa kulazimishwa," mkuu wa Chama cha Wanasheria wa Nigeria Mazi Afam Osigwe alisema. "Wakati ambapo raia wanalazimishwa kupiga kura chini ya tishio la kufungwa, kiini kizima cha uchaguzi huru na wa haki kinaporomoka."

Mwanasheria mashuhuri wa Nigeria alisema "haitawezekana kabisa kuwashtaki mamilioni ya Wanigeria ambao wanaweza kuamua kususia uchaguzi wa kitaifa na wa serikali za mitaa ambao umeshushwa hadhi yake kuwa kurejesha madarakani utawala mbovu, ufisadi, na matumizi mabaya ya madaraka kwa muda na wanachama wa tabaka la kisiasa."

Chini ya nchi nyingine 20 hutekeleza upigaji kura wa lazima, kulingana na tume ya uchaguzi nchini Australia ambapo upigaji kura wa lazima ni mhimili mkuu wa kura za kitaifa tangu 1925.

Idadi kubwa ya wapiga kura nchini Australia

Wapiga kura wanaoshindwa kupiga kura siku ya uchaguzi wanatozwa faini ya dola 20 za Australia ($13 USD), adhabu ndogo lakini yenye ufanisi.

Wapiga kura hawajawahi kupungua chini ya asili mia 90 nchini Australia.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us