AFRIKA
2 dk kusoma
Rwanda yafanya makubaliano ya usafiri wa anga na nchi 12
Mikataba ya huduma za anga ya nchi mbili ni mikataba inayoruhusu huduma za kimataifa za usafiri wa anga za kibiashara kati ya maeneo yao.
Rwanda yafanya makubaliano ya usafiri wa anga na nchi 12
Rwandair imefanya mikataba na nchi 12 za huduma ya ndege/ Picha: Reuters
27 Mei 2025

Rwanda imeidhinisha makubaliano ya huduma za anga kati yake na serikali za nchi 12.

Haya yalipitishwa na kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais Paul Kagame, Jumatatu, Mei 26.

Nchi hizo ni pamoja na Eswatini, Guinea, Liberia, Malawi, Mali, Zimbabwe, Georgia, Ufaransa, Poland, Oman, Suriname, na Canada

Mikataba ya huduma za anga ya nchi mbili ni mikataba inayoruhusu huduma za kimataifa za usafiri wa anga za kibiashara kati ya maeneo yao.

Mikataba hii inarahisisha usafirishaji wa watu, bidhaa, mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na inakusudiwa kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kukuza utalii.

Ingawa uidhinishaji huu hauhusishi urushaji wa ndege mara moja, unawezesha mashirika ya ndege kama vile RwandAir kujadili haki za njia na kuanzisha huduma mpya mara tu masharti yote ya udhibiti na kibiashara yanapofikiwa.

Hatua hiyo inawiana na mkakati wa Rwanda wa kuwa kitovu cha usafiri wa anga katika bara na kimataifa, ikiungwa mkono na miradi mikubwa ya miundombinu kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bugesera na uwekezaji wa muda mrefu katika Shirika la Ndege la Kitaifa, RwandAir.

Rwanda tayari imetia saini jumla ya makualiano 108 na nchi mbalimbali duniani.

Hii inajumuisha mikataba 49 na mataifa ya Afrika, 25 na nchi za Ulaya, 19 na nchi za Mashariki ya Kati na Asia, na 15 na mataifa katika Amerika.

/

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us