AFRIKA
1 dk kusoma
Mkanyagano wasababisha vifo vya watoto 29 Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wengi wao wamefariki katika eneo la tukio baada ya mlipuko ndani ya shule kusababisha mkanyagano.
Mkanyagano wasababisha vifo vya watoto 29 Jamhuri ya Afrika ya Kati
Tukio hilo lilitokea katika shule moja ya upili mji mkuu, Bangui. / Getty
26 Juni 2025

Mlipuko na mkanyagano ulisababisha vifo vya wanafunzi wa shule 29 na wengine zaidi ya 250 kujeruhiwa katika shule moja mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mamlaka zimesema siku ya Alhamisi.

Mlipuko huo ulitokea Jumatano katika Shule ya Upili ya Barthelemy Boganda mjini Bangui wakati umeme ulipokuwa unarudishwa kutokana na mtambo mmoja kuwa na hitilafu ndani ya shule, kulingana na Wizara ya Elimu.

Wengi ya waliofariki – ikiwemo wasichana 16 – ilitokea katika eneo la tukio kutokana na mkanyagano huku wengine wakithibitishwa kufariki walipofika hospitali, Wizara ya Afya imesema katika taarifa.

Watu wasiopungua 260 walijeruhiwa na wanaendelea kutibiwa katika hospitali mbalimbali, wizara imesema.

Inakadiriwa kulikuwa na wanafunzi kama 5,000 katika shule hiyo wakati wa ajali.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us