AFRIKA
2 dk kusoma
Faru sabini weupe kutoka Afrika Kusini wapelekwa Rwanda
Rwanda inasema faru weupe 70 wamesafirishwa salama hado katika taifa hilo la Maziwa Makuu baada ya safari ya siku mbili ya kilomita 3,000 kutoka Afrika Kusini.
Faru sabini weupe kutoka Afrika Kusini wapelekwa Rwanda
Faru wa kusini mweupe sasa ameorodheshwa kama walio kwenye ‘’hatari ya kuangamia’’, ikiwa wamebaki 17,000 pekee. / Picha: Reuters
10 Juni 2025

Rwanda imesema siku ya Jumanne kuwa Faru 70 wamesafirishwa katika taifa hilo la Maziwa Makuu baada ya safari ya siku mbili ya kilomita karibu 3,000 kutoka Afrika Kusini.

Huu ulikuwa usafirishaji mkubwa zaidi wa faru, ambapo mmoja anaweza kuwa na uzani wa hadi tani mbili, maafisa wa Rwanda wamesema.

Wakati mmoja walikuwa wengi sana kote kusini mwa jangwa la sahara, sasa hivi idadi ya faru imepungua kutokana na uwindaji wa wakoloni wa kizungu na ujangili.

Wanyama hao walisafirisha kwa safari mbili 35 – walipandishwa ndege aina ya Boeing 747, kisha kwa njia ya barabara – kutoka mbuga ya Afrika Kusini ya Munywana hadi ile ya Akagera nchini Rwanda, au kama kilomita 3,000 hivi, kulingana na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB).

Uangalizi wa makini

Kutakuwa na "kundi la madaktari wa wanyama ambalo litaangalia afya zao na mienendo yao kwa wiki kadhaa kuhakikisha kuwa hawapati tatizo lolote kutokana na kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine", ilisema katika taarifa.

Hatua hii ilikuwa sehemu ya mradi wa mbunga za Afrika, ukiungwa mkono na Wakfu wa Howard G. Buffett, na wenye lengo la kuunga mkono kuimarishwa kwa idadi ya wanyama hao na kuwapa fursa ya kuzaliana nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa Wakfu wa Kimataifa wa Faru (IRF), ujangili wa faru barani Afrika umeongezeka kwa 4% kutoka 2022 hadi 2023, huku faru wasiopungua 586 wakiwa wameuawa 2023.

Faru mweupe wa kusini, ni moja kati ya aina mbili, na sasa ameorodheshwa kama "aliye katika hatari ya kuangamia", idadi yao ikiaminika kuwa wamebaki 17,000, kulingana na shirika la IUCN.

Faru mweupe wa kaskazini ameangamia kabisa, na wamebaki faru wawili majike ambao wako hai.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us