AFRIKA
2 dk kusoma
Papa Francis na ujumbe wake wa amani Afrika
Barani Afrika ametambuliwa kama papa wa ujumbe wa amani ikiwa amezuru nchi tofdauti katika awamu wake wa uongozi.
Papa Francis na ujumbe wake wa amani Afrika
Papa Francis alizuru Sudan Kusini na kuhi,miza amani / Reuters
21 Aprili 2025

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis ni raia wa Argentina na ndiye kiongozi wa kwanza kutokea nchi zinazoangaliwa kuwa zinaendelea , kama Afrika , Asia na latin Marekani .

Novemba  2015 Papa Francis alizuru Kenya .

Nchi hiyo ilikuwa imekumbwa na mashambulizi ya kigaidi 2013 na 2014 ambapo watu waliauwa kinyama .

Katika ziara yake alitembelea eneo la makazi duni la kangemi jijini Nairobi ambapo aliongolewa kuhusu uwepo wa ukoloni mambo leo.

Mwezi huo huo Novemba 2015 Papa Francis alienda Uganda kwa ziara ya siku tatu.

Mbali na ibada kuu alikutana na vijana, akatembelea kituo cha kutoa misaada na kukutana na viongoi wa kidini nchini humo.

Wakati amabapo vita vya kindani katika jamhutri ya Afria ya Kati ilikuwa imenoga , Papa francis alitembela nchi hiyo .

Mzozo nchini humo ulihusisha kwa vikubwa mvutano wa kidini na ulianza 2013 baada ya rais wa nchi hiyo François Bozizé  kuondolewa na waasi kwa mapinduzi.

Maelefu waliuawa na zaidi ya watu milioni moja kuripotiwa kulazimika kuyahama makazi yao.

Mwaka wa 2017 alizuru Misri ambapo alihimiza umoja huku mzozo wa kidini uliathiri mania nchini humo .

Ilikuwa mara ya kwanza kwa papa huyo kutembelea nchi iliyo katika mzozo.

Machi 2019 akaenda Morocco kuhimiza amani baada ya mgogor wa kidini pia.

Ujumbe wake wa amani ulimpeleke Sudan Kusini Februari 2023. Nchi hiyo ilikumbwa na vita kuanzia 2013 miaka miwili tu baada ya kupata uhuru.

Mwaka 2019 Papa Francis aliwakaruibisha viongozi wa Sudan Kusini waliokuwa wakizozana,  rais Salva kiir na makamu wake wa Riek Machar, akawabusu miguu na kuwasihi kuacha vita.

Vatican pia ilichangia kwa kuwa mweneyji wa maongezi ya amani ya Sudan Kusini.

Ziara ya Papa Francis DRC

Kutoka 31 Januari hadi  3 Februari 2023 Papa Francis alizuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  aliposhutumu "sumu ya uchoyo" inayosababisha aliyosema inasababisha migogoro barani Afrika.

Aliashiria kuwa madini nchini DRC imekuwa chanzo cha mgogoro alisema ulimwengu tajiri unapaswa kutambua kwamba watu ni wa thamani zaidi kuliko madini yaliyo chini yao.

Mipango yake kufika Kivu Kaskazini haikufaulu kwasababu mashambulizi ya kikundi cha waasi wa M23 yalikuwepo.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us