30 Machi 2025
Akiwa ameinukia katika hali ngumu ya kutengwa licha ya kuwa mwana wa mfalme wa Zulu, Shaka kaSenzangakhona alipata mafunzi kabambe ya kivita.
Aliweza kubuni mbinu na silaha mpya pamoja na kuwa na nidhamu isiyo na kifani.
Ubunifu wake wa kivita na uongozi wake katika kupigana ulibadilisha historia ya Wazulu na kumpandisha cheo hadi kuwa mfalme, lakini huzuni ya kumpoteza mamake ulimponza na kusababisha maadui wake kuchukua nafasi kummaliza pamoja na utawala wake.