Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov wamesisitiza dhamira moja ya pamoja ya nchi zao kuhakikisha kuwa mipaka ya Syria inaheshimiwa na kuendeleza ustawi wa kikanda wa muda mrefu.
“Tukiwa kama Uturuki na Urusi, tutaendelea kufanya kazi pamoja kuhakikisha kuwa mipaka ya Syria inaheshimiwa na uhuru wao unalindwa,” Fidan alisema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jijini Moscow.
“Tutaendeleza juhudi zetu, kuhakikisha kuwa watu wa Syria wanapata mafanikio na ustawi.”
Wanadiplomasia hao wawili waandamizi wameashiria nia yao ya kuanzishwa kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine — wote wakiunga mkono jukumu za Uturuki kama mpatanishi anayeaminika.
“Tunaweza kuwaomba tena marafiki zetu wa Uturuki kwa hatua ya pili ya majadiliano na Ukraine,” Lavrov alisema, akieleza jiji la Istanbul kama “sehemu ya matumaini” kwa mazungumzo katika siku za baadaye.
Uturuki iliwezesha mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine katika kipindi cha miaka mitatu jijini Istanbul 16 Mei, ambapo pande zote mbili zilikubaliana kubadilishana wafungwa wengi zaidi watu 1,000 kutoka kila upande na kuendelea na mazungumzo kwa lengo la kusitisha kabisa mapigano.
“Kumaliza vita kabisa ni lengo letu la pamoja”
Mawaziri hao wawili wa mambo ya nje walikutana katika siku ya pili ya ziara ya kikazi ya Fidan jijini Moscow ambapo awali alikuwa amekutana na msaidizi wa rais wa Urusi Vladimir Medinsky, kiongozi wa ujumbe wa Urusi katika mazungumzo ya Urusi na Ukraine yaliyofanyika jijini Istanbul 16 Mei, na pia Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Kwa mara nyingine tena Fidan alisisitiza utayari wa Uturuki kuwa wenyeji wa mazungumzo yoyote katika siku zijazo kati ya Urusi na Ukraine na kutoa pongezi kwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa kuratibu mchakato huo.
Fidan aliunga mkono utayari wa Lavrov kwa mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine, akisisitiza nafasi ya Uturuki kimaeneo na kisiasa katika kumaliza vita hivyo.
“Tunaishi katika eneo moja … kumaliza vita hivi kabisa ni lengo letu la pamoja, na Uturuki itaendelea kuunga mkono juhudi hizo za kumaliza vita hivyo,” Lavrov alisema.
Kuhusu mzozo wa Gaza, Fidan alitoa onyo kali kuhusu athari za kuendelea kwa machafuko hayo.
“Mauaji ya halaiki Gaza lazima yaishe mara moja,” alisema. “La sivyo, vurugu zitakazoikumba Israeli hazitoweza kusimamishwa.”
Lavrov alisisitiza ushirikiano wake na Uturuki kuhusu suala la Palestina. “Tuna maoni sawa na Uturuki kuhusu suala la Palestina. Kinachoendelea Gaza na Ukingo wa Magharibi hakikubaliki,” alisema.
Ziara ya Fidan jijini Moscow imefanyika tarehe 26–27 Mei baada ya kualikwa na Lavrov, kwa mujibu wa vyanzo vya wizara ya mambo ya nje ya Uturuki.
Wakati wa ziara hiyo, Fidan alipokewa na Rais wa Urusi Vladimir Putin na kufanya mazungumzo na Lavrov. Pia alikutana na viongozi kadhaa waandamizi wa Urusi, ikiwemo msaidizi wa rais Vladimir Medinsky — ambaye aliongoza ujumbe wa Urusi katika mazungumzo ya Urusi na Ukraine jijini Istanbul 16 Mei.
Uturuki iliratibu mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine katika kipindi cha miaka mitatu jijini Istanbul 16 Mei, ambapo pande zote mbili zilikubaliana kubadilishana wafungwa wengi zaidi ya watu 1,000 kutoka kila upande na kuendelea na mazungumzo ya kusitisha kabisa mapigano.