Namna mafanikio ya Rwanda yanavyohusishwa na Rais Paul Kagame
Namna mafanikio ya Rwanda yanavyohusishwa na Rais Paul Kagame
Nchi ya Rwanda inasifika kwa mambo kadhaa, kubwa ikiwa ni mazingira yake yaliyo safi na usalama kwa kiasi kikubwa.
25 Juni 2025

Mafanikio yote hayo ya nchi yanatajwa kuwa ni sera za serikali ya Rais Paul Kagame ambae ameshika hatamu ya nchi hiyo tangu mwaka 2000 baada ya kujiuzulu kwa rais aliyekuwa madarakani wakati huo Pasteur Bizimungu.

Kagame alizaliwa miaka 67 iliyopita nchini Rwanda na akiwa mdogo familia yake ilienda uhamishoni nchini Uganda.

Sehemu kubwa ya maisha yake na harakati zake zilikuwa nchini Uganda.Katika miaka ya themanini alijiunga na kundi la rais wa Uganda wa sasa Yoweri Museveni, kumsaidia katika harakati zake za kijeshi.

Baadae Kagame alijiunga na Rwanda Patriotic Front (RPF) wapiganaji wa Rwanda na akawa kiongozi wao mwaka 1990.

 Baada ya kumalizika kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, kuliundwa serikali kwa misingi ya kile kilichojulikana kama makubaliano ya Amani ya Arusha na Paul Kagame akawa Makamu wa rais na pia waziri wa ulinzi, huku Pasteur Bizimungu akiwa rais wa nchi.

Kwa wadhifa huo ina maana alikuwa anasimamia jeshi la taifa hilo.Walianza kutofautiana hadharani na aliyekuwa rais Bizimungu, hadi Bizimungu akaamuwa kujiuzulu 2000.

Tangu kuingia madarakani wakati huo, Kagame ameshiriki katika uchaguzi 2003, 2010, 2017 na 2024.Mara zote hizo akishinda kwa kishindo, kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura.

Katiba inamruhusu kusimama tena kwa muhula mwingine.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us