AFRIKA
1 dk kusoma
Waasi wa M23 wadaiwa kuwafanyisha kazi wachimba dhahabu bila malipo
Mwezi Mei mwaka huu, kampuni hiyo ilidai kuwa iliamriwa kusitisha uchimbaji wa dhahabu baada ya waasi wa M23 kuituhumu kukwepa kodi.
Waasi wa M23 wadaiwa kuwafanyisha kazi wachimba dhahabu bila malipo
Mgodi wa dhahabu nchini DRC./Picha:Wengine
30 Juni 2025

Kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu nchini DRC, Twangiza Mining SA imewashutumu waasi kwa kuwalazimisha wachimba madini kwenye mgodi mmoja nchini humo kufanya kazi bila malipo.

Hii ni baada ya waasi hao kudhibiti mgodi huo unaopatikana kusini kwa jimbo la Kivu, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Mwezi Mei mwaka huu, kampuni hiyo ilidai kuwa iliamriwa kusitisha uchimbaji wa dhahabu baada ya waasi wa M23 kuituhumu kukwepa kodi.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini DRC, ilisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wake walikuwa wakishikiliwa mateka na kushurutishwa kufanya kazi katika mazingira magumu bila malipo.

CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us