Umoja wa Mataifa umelaani mauaji ya Mahelet Sitotaw Abera, mfanyakazi wa kibinadamu ambaye aliuwawa wakati wa mapigano kati ya vikosi vya serikali na vikundi visivyo vya serikali.
Tukio hilo lilitokea Juni 20, 2025 katika wilaya ya Angot, iliyoko ukanda wa Wollo Kaskazini katika mkoa wa Amhara nchini Ethiopia.
Mzozo huko ulianza chini ya mwaka mmoja baada ya vita vya eneo la Tigray, vilivyomalizika mnamo 2022.
Amhara ni moja ya makabila yenye mchango mkubwa nchini Ethiopia.
Mzozo wa Amhara ulianza kama mapigano madogo ya hapa na pale kati ya vikosi vyenye silaha na vikosi vya serikali mnamo Aprili 2023.
Hata hivyo, yalizidi kuongezeka kwa kasi na kugeuka kuwa uasi miezi minne baadaye baada ya vikosi vinavyojulikana kama Fano, kufanya mashambulizi kwa nia ya kudhibiti miji mikubwa katika eneo hilo.
Kufikia sasa, ghasia hizo zimesababisha mauaji ya zaidi ya watu 100,000 na kuwafanya watoto milioni 4.7.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, Mahelet alikuwa akisaidia katika ukusanyaji wa takwimu za kibinadamu wakati alipouwawa.