AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania kuwarudisha raia wake 42 waliokwama Israel
Mchakato huo wa kuwarudisha Watanzania hao, uliratibiwa na Wizara ya Mambo Nje ya Tanzania, chini ya maelekezo ya rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan.
Tanzania kuwarudisha raia wake 42 waliokwama Israel
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mahmoud Thabit Kombo./Picha:Wengine
25 Juni 2025

Raia 42 wa Kitanzania waliokwama nchini Israel, kufuatia mzozo unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, wanatarajia kuwasili Juni 25, 2025, serikali ya nchi hiyo imesema.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, raia hao watarudi katika makundi tofauti, wakitumia shirika la ndege la Ethiopia.

 

Taarifa hiyo, iliongeza kuwa kundi la kwanza la raia hao litawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kundi la pili lilitegemewa kuwasili JNIA, majira ya saa kumi na moja jioni (kwa saa za Afrika Mashariki).

Mchakato huo wa kuwarudisha Watanzania hao, uliratibiwa na Wizara ya Mambo Nje ya Tanzania, chini ya maelekezo ya rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan.

 “Serikali ya Tanzania iko tayari kutoa ulinzi kwa raia wake, popote pale walipo ulimwenguni,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us