UTURUKI
2 dk kusoma
Maelfu waandamana kupinga mashambulizi ya Israeli Gaza
Jijini Istanbul kumefanyika maandamano yaliyotoa wito wa kutaka kusitishwa kwa mapingano yanayoendelea Gaza, Palestina, huku washiriki wakitaka hatua zaidi kutoka mataifa ya Kiislamu na kulaani ukimya wa dunia.
Maelfu waandamana kupinga mashambulizi ya Israeli Gaza
Maandamano haya yanafanyika huku dunia ikishuhudia ongezeko la wanaopiga kampeni za kijeshi za Israeli Gaza, ambazo zimesababisha kufanyika kwa maandamano katika nchi kadhaa, ikiwemo Uturuki. / AA
21 Aprili 2025

Maelfu ya watu wamekusanyika jijini Istanbul katika wilaya ya Uskudar kulaani mashambulizi ya Israeli yanayoendelea Gaza, katika maandamano waliyoyaita “Gaza inakufaa! Amkeni!” yaliyoandaliwa na makundi ya kutetea haki za binadamu.

Maandamano hayo yamefanyika siku ya Jumapili, ambapo makundi yalielekea katika Uwanja wa Uskudar kupinga mashambulizi ya Israeli huko Gaza, ambayo tayari yameua maelfu ya watu tangu Oktoba 7, 2023.

Waandamanaji walipeperusha bendera za Uturuki na Palestina, huku wakiimba maneno kama vile, “Aangamie dhalimu Israeli” na wengine kubeba mabango yaliyoandikwa “50,800+ wameuawa mashahidi Palestina,” na “Vizuizi Gaza ni haramu.”

Washiriki pia wameonyesha mshikamano na watu wa Gaza, huku wazungumzaji wakitaka mataifa ambayo sio ya Waislamu kupinga kila walichokiita uhalifu wa kivita wa Israeli dhidi ya ubinadamu.

Akihutubia waliojumuika, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya IHH ya Misaada ya Kibinadamu Ahmed Goksun amelaani mauaji ya Israeli, na kusema nchi hiyo imetangaza ukatili kwa ulimwengu kupitia mashambulizi ya Gaza.

“Sitisha huu ukatili, haya mauaji ya halaiki sasa,” amesema.

Goksun ameulaumu ulimwengu wa Kiislamu kwa kugawanyika katika “uoga na washirika,” na kutahadharisha kwamba kutochukua hatua kutakuwa na athari mbaya.

“Wale washirika siku moja watahukumiwa,” amesema.

“Kwa waoga, tunauliza-hamna hata ujasiri wa mtoto aliyesimama mbele ya kifaru Gaza?”

Maandamano haya yanafanyika huku dunia ikishuhudia ongezeko la wanaopiga kampeni za kijeshi za Israeli Gaza, ambazo zimesababisha kufanyika kwa maandamano katika nchi kadhaa, ikiwemo Uturuki.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us