Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania (CHADEMA) wamelitaka Jeshi la Magereza nchini humo pamoja na vyombo vingine vya dola kueleza alipo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Lissu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa Aprili 18, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Brenda Rupia, kwa nyakati tofauti, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar Ali Ibrahim Juma, wanachama, mawakili na wanafamilia wamefika katika Gereza la Keko jijini Dar es Salam, ambako anashikiliwa, bila kumuona.

Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele amesema kuwa wao kama tume wametafsiri sheria hiyo wanavyojua wao, na iwapo CHADEMA wana tafsiri tofauti ni haki yao, ila waachie uamuzi wa mwisho mahakama.
“Hata hivyo, juhudi zao za kumuona Mheshimiwa Lissu hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa hayupo katika gereza hilo, cha kusikitisha, hawakupewa maelezo yoyote rasmi juu ya alipopelekwa,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Lissu anashikiliwa katika gereza la Keko kwa tuhuma za Uhaini zinazomkabili.