22 Aprili 2025
Siku ya Jumanne rais wa Ghana John Dramani Mahama amemsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi wakisubiri matokeo ya uchunguzi dhidi yake, taarifa ilisema.
Jaji Gertrude Torkornoo aliapishwa kuwa Jaji Mkuu Juni 2023. Aliongoza hafla ya kuapishwa kwa Rais Mahama kwa muhula wake wa pili mwezi Januari.
Malalamiko rasmi matatu yamewasilishwa kutaka aondolewe ofisini.Hata hivyo madai dhidi yake hayajafahamika wazi kwa umma.
Rais Mahama ana sababu za kuamini kuwepo kwa ushahidi wa kutosha kwa madai yaliyowasilishwa, taarifa kutoka ofisi ya rais ilisema.
Ameteua kamati ya watu watano kuchunguza madai hayo.