ULIMWENGU
2 dk kusoma
Kenya yaorodheshwa na Ulaya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya ulanguzi wa fedha
Nchi inayowekwa katika orodha hii inamaanisha kuwa mashirika ya kifedha zikiwemo benki zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala inayohusisha nchi zilizotengwa, kwa kuongeza hatua za udhibiti.
Kenya yaorodheshwa na Ulaya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya ulanguzi wa fedha
Tume ya Ulaya imesema inakinga soko lake la ndani kwa kuchunguza uhalali wa mifumo ya fedha duniani/ Picha: Getty / Getty Images
12 Juni 2025

Tume ya Ulaya imeziweka nchi kadhaa za Afrika katika orodha yake ya nchi zenye mapungufu ya kimkakati katika kupambana na ulanguzi wa fedha haramu na kukabiliana na ufadhili wa serikali za ugaidi (AML/CFT).

Nchi zilizowekwa sasa katika uangalizi mkubwa na Ulaya ni pamoja na Algeria, Angola, Côte d’Ivoire na Kenya.

Hii inamaanisha kuwa mifumo ya kifedha ya Umoja wa Ulaya inayosimamiwa na mfumo wa kupambana na ulanguzi wa fedha inatakiwa kutumiwa kwa makini na kuimarishwa katika shughuli zinazohusisha nchi hizi.

“Hii ni muhimu ili kulinda mfumo wa fedha wa EU,” Tume ya Ulaya imesema katika taarifa.

Uchunguzi huo una nia ya kupambana na mzunguko wa kimataifa wa fedha usio halali.

Wakati huo Senegal na Uganda ni kati ya nchi ambazo zimeondolewa katika orodha hiyo.

Utambulisho wa nchi zilizo na hatari kubwa unahitajika ili kulinda mfumo wa kifedha wa EU na utendaji kazi mzuri wa soko la ndani,” Tume ya Ulaya imeelezea katika tovuti yake.

“EU imepewa uwezo wa kutambua nchi zenye hatari kubwa ambazo zina mapungufu ya kimkakati katika kupambana na ulanguzi wa pesa na kukabiliana na ufadhili wa mifumo ya ugaidi. Hii inapunguza hatari zinazoweza kuleta vitisho kwa mfumo wa kifedha wa Muungano,” EU imeongeza kusema.

Nchi nyengine katika orodha ya nchi zenye hatari ya ulanguzi wa fedha ni Burkina Faso, Cameroon, DRC, Mali, Mozambique, Nigeria, Afrika Kusini, Sudan Kusini na Tanzania.

Nchi ikiwekwa katika orodha hii inamaanisha kuwa mashirika ya kifedha zikiwemo benki zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala inayohusisha nchi zilizotengwa, kwa kuongeza hatua za udhibiti.

Ili kupambana kwa ufanisi na mzunguko wa kimataifa wa fedha chafu, jitihada za kimataifa zinahitajika.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us