Israel na Iran wamekuwa wakibadilishana mashambulio katika vita vipya vilivyoanzishwa kwa uchokozi na Israel.
Israel ilianza kwa kulipua maeneo kadhaa ya kijeshi ya Iran lakini pia maeneo ya Nyuklia, ambayo kimsingi ndio ilikuwa lengo lao hasa. Kusitisha maendeleo ya Iran ya urutubishaji wa madini ya Urania.
Israel inadai kuwa Iran inaendeleza mpango wa kutengeneza mabomu ya Nyuklia na imekaribia kukamilisha, jambo ambalo Iran Inakanusha.
Lakini kwa kulenga na kulipua maeneo haya ya Nyuklia, kuna weza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na mazingira ya muda mfupi na muda mrefu.
Tishio kwa eneo zima
Athari hizi zinaweza kuathiri sio Iran pekee bali pia nchi jirani na eneo zima.
Hatari hutofautiana kulingana na ikiwa mashambulizi yalisababisha kuvuja kwa mionzi hatari a radiolojia, uchafuzi wa kemikali au uharibifu mwingine wa miundombinu.
Ni zipi baadhi ya hatari kwa afya zinazowezekana?
Ugonjwa mkali wa papo kwa hapo kwa waathiriwa kutokana na kupumua hewa yenye mionzi, Hatari za muda mrefu kama saratani haswa tezi, mapafu, na leukemia.
Uchafuzi wa mazingira
Uharibifu wa maumbile na kasoro za kuzaliwa katika vizazi vijavyo kutokana na uharibifu ya Jeni.
Pia uvujaji unaweza kuathiri ubora wa hewa na kuingia kwenye mzunguko wa chakula kupitia mazao au mifugo iliyoambukizwa.
Kulingana na mifumo ya upepo, chembechembe za miale zinaweza kusambaa kuvuka mipaka mfano hadi nchi jirani za Iraq, Afghanistan, au majimbo ya Ghuba ya Uajemi.
Madhara mengine ni uchafuzi wa mazingira kupitia maji ya ndani ya ardhi na maji ya juu ya ardhi kama mabwawa, mito na bahari.
Majanga ya Fukushima na Chenorbyl
Haya yakitokea inamaanisha pia kulemewa mifumo ya huduma za afya na kulazimika watu kuyahama makazi yao kwa muda mrefu kwani huchukua miaka mingi kabla uchafuzi huo kusafishwa.
Hatari hizi zishatokea kwa mfano katika janga la Fukushima nchini Japan mwaka 2011 au Chenorbyl ya Urusi ambayo miaka arobaini baadaye, bado mkasa huo haujasafishwa na athari zake zinazidi kuonekana.
Kwa hiyo ikiwa kweli Iran inacho kiwango cha juu cha madini ya Urania kama inavyodaiwa, Wataalamu wanaonya Israel yatakiwa kuwa mwangalifu zaidi kwa namna inarusha mabomu yako.