MICHEZO
1 dk kusoma
Brazil yaendeleza rikodi ya kipekee ya kushiriki kila toleo la Kombe la Dunia
Mbali na Brazil, timu nyingine kutoka Amerika Kusini ambazo tayari zimefuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 ni Argentina na Ecuador.
Brazil yaendeleza rikodi ya kipekee ya kushiriki kila toleo la Kombe la Dunia
Mabingwa hao wa kihistoria mara tano sasa wanatarajiwa kucheza michuano yao ya 23 ya Kombe la Dunia / Reuters
11 Juni 2025

Brazil imefuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Paraguay katika mechi iliyochezwa mjini São Paulo, ushindi uliompa Carlo Ancelotti mafanikio yake ya kwanza kama kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa.

Mshambulizi wa Real Madrid, Vinícius Jr., alifunga bao pekee la mchezo kipindi cha pili, akimalizia pasi safi kutoka kwa Matheus Cunha, mchezaji ambaye amenunuliwa na Manchester United hivi majuzi.

Ushindi huo, ambao ni wa kwanza kwa Ancelotti kufuatia sare tasa ya 0-0 dhidi ya Ecuador katika mechi yake ya kwanza wiki iliyopita, umeihakikishia Brazil nafasi ya kuendeleza rekodi yao ya kipekee ya kushiriki kila toleo la Kombe la Dunia.

Mabingwa hao wa kihistoria mara tano sasa wanatarajiwa kucheza michuano yao ya 23 ya Kombe la Dunia, itakayofanyika mwaka ujao nchini Marekani, Canada na Mexico.

Mbali na Brazil, timu nyingine kutoka Amerika Kusini ambazo tayari zimefuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 ni Argentina na Ecuador.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us