Ihram katika Hajj: Kwa nini mahujaji wa Kiislamu huvaa shuka jeupe?
ULIMWENGU
3 dk kusoma
Ihram katika Hajj: Kwa nini mahujaji wa Kiislamu huvaa shuka jeupe?Takriban Waislamu milioni mbili kutoka kote duniani wanatazamiwa kuhudhuria ibada ya Hajj ya mwaka huu nchini Saudi Arabia. Jambo moja la kuvutia zaidi ni shuka jeupe linalovaliwa na mahujaji linalojulikana kama Ihram.
Muslims perform morning prayers in the Grand Mosque during the annual Hajj pilgrimage in the holy city of Mecca / Reuters
3 Juni 2025

Mahujaji wanapovaa vazi takatifu la Ihram, wanaanza safari ya kiroho ya umoja, usawa, na kujitolea.

Sheikh Aminu Ibrahim Daurawa, mwanachuoni wa Kiislamu nchini Nigeria, anasema kuna sababu kadhaa kwa nini mahujaji kuvaa ihram nyeupe.

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ujumla alihimiza uvaaji wa nguo nyeupe, kwa kuwa inaashiria usafi wa ndani na nje, mwanachuoni huyo wa Kiislamu anaiambia TRT Afrika.

"Mtume Muhammad (S.A.W) amehimiza uvaaji wa nguo nyeupe hata katika siku za kawaida. Amesema: 'Muvae nguo nyeupe na mufinike maiti zenu sanda nyeupe'," Sheikh Daura anaeleza.

Hadithi hii inaangazia umuhimu wa vazi jeupe katika mila ya Kiislamu.

Nguo nyeupe hutumika kama ukumbusho wenye nguvu kuonyesha umoja wa mahujaji na lengo la kiroho.

"Rangi nyeupe huonyesha usafi au uchafu zaidi. Mtu akivaa kitambaa cheupe, hali yake ya usafi itatambulika kwa urahisi kulingana na jinsi anavyoonekana," Sheikh Daurawa, ambaye pia anafanya ibada ya Hija ya mwaka huu, anafafanua.

Hii inadhihirisha umuhimu wa usafi na kuwa hali ya kawaida katika vazi la Ihram.

Usawa na unyenyekevu

Vazi la Ihram linavuka hadhi ya kijamii, mali, na mafanikio ya kidunia, likisisitiza usawa wa asili wa waumini wote.

Sheikh Daurawa anabainisha, "Ihram pia hutumika kama sare ambayo inafanya kuwa vigumu kutofautisha kati ya tajiri na maskini, na kati ya viongozi na raia wao."

Umoja huu ni kipengele cha msingi cha Hajj, kuruhusu mahujaji kusimama sawa mbele ya Mungu.

‘’Kama watu wangeruhusiwa kuvaa nguo zao za kawaida, mtu anaweza kuvaa mavazi ya kifalme, mavazi ya kuonyesha uongozi, kuvaa kama msomi, au hata kuvaa nguo za maskini,’’ Daurawa anasema.

‘’Katika hali hiyo, watu hawangekuwa wanyenyekevu; kungekuwa na kiburi na majivuno. Watu wangeonyesha mavazi yao. Walakini, kwa kuwa sasa ni sare, hakuna tofauti. Inaonyesha kuwa watu wako sawa mbele ya Mwenyezi Mungu, ila watakua wanatofautiana katika ucha Mungu,’’ mwanazuoni huyo wa Kiislamu anaongeza.

Wakati wa kuanza kuvaa Ihram

Vazi la Ihram huvaliwa kwa muda wote wa ibada za Hajj. Mahujaji kwa kawaida huvaa vazi jeupe kabla ya kuingia katika mipaka ya Ihram, kwa kawaida kwenye maeneo maalum ya Meeqat karibu na Makka au kwenye hoteli au makazi yao ikiwa wako Makka, siku ya 8 ya Dhu al-Hijjah.

Baada ya kumaliza ibada ya Hajj, mahujaji wanaweza kutoa vazi la Ihram baada ya kutekeleza ibada ya kupiga mawe Jamarat (Shetani) na hapo wanaruhusiwa kunyoa au kupunguza nywele zao katika siku ya 10 au 11 ya Dhu al-Hijjah.

Hii inaashiria mwisho wa Ihram, na mahujaji wanaweza kuvaa mavazi yao ya kawaida.

Zaidi ya umuhimu wake wa kiroho, vazi jeupe pia linawakilisha kujitolea kwa utakaso wa kiroho. Mahujaji wanaposafiri kwenye ibada za Hajj, nguo nyeupe huwakumbusha kuzingatia kwao juu ya uwepo wa Mungu.

Muundo na sheria

Sheikh Daurawa anaongeza kusema, "Inawakumbusha kifo na kuwakumbusha kusimama mbele ya Mungu." Vazi la Ihram ni vazi la kawaida, jeupe, lisilo na mshono linalovaliwa na mahujaji wakati wa Hajj.

Kwa wanaume, kwa kawaida huwa na shuka mbili: Izār (vazi la chini) ambalo huzungushiwa kiunoni na vazi la juu ambalo huning'inia kwenye bega, mara nyingi bega la kulia huwekwa wazi. Muundo huo unasisitiza urahisi, unyenyekevu, na usawa miongoni mwa mahujaji.

Wakiwa wamevaa Ihram, mahujaji hawawezi kushiriki katika shughuli kama vile kuwinda, kunyoa nywele kukata kucha, au kufanya ngono. Ni lazima pia waepuke kubishana, kupigana, au kujionyesha.

Wanaume hawaruhusiwi kufunika vichwa vyao, na wanaume na wanawake wanatarajiwa kudumisha kiasi kiasi kikubwa cha unyenyekevu, wakizingatia ujitoaji wa kiroho.

Rangi nyeupe inaashiria usafi na umoja. Mavazi ya wanawake hutofautiana, lakini kwa kawaida huvaa mavazi yasiyo onyehsa mapambo , yasiyobana ambayo hufunika miili yao, isipokuwa uso na mikono yao.

Wanawake wanaruhusiwa kuvaa nguo wanazopenda, kwa miongozo fulani, Daurawa anasema.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us