AFRIKA
1 dk kusoma
Uuzaji wa kahawa ya Ethiopia nje ya nchi waongezeka kwa zaidi ya asilimia 40
Mamlaka zinasema kuwa haki za kuuza kahawa nje ya nchi pia zilipewa wakulima waliokuwa na leseni, kuwawezesha zaidi ya 100 miongoni mwao kuuza kahawa nje ya nchi.
Uuzaji wa kahawa ya Ethiopia nje ya nchi waongezeka kwa zaidi ya asilimia 40
Wakulima zaidi ya 100 wameruhusiwa kuuza kahawa nje ya nchi. / Getty Images
1 Julai 2025

Ethiopia imeimarisha uuzaji wake wa kahawa nje ya nchi, na kufanikiwa kupita malengo yake pamoja na kupata fursa ya kuingia katika masoko mapya 20 ya kimataifa ndani ya kipindi cha miezi 11, serikali imetangaza.

Bodi ya Kahawa na Chai ya Ethiopia (ECTA) iliripoti kuwa nchi hiyo iliuza nje ya nchi tani 409,605 za kahawa, ikiwa ni zaidi ya kiwango walichotarajia cha tani 280,887.

Shafi Umer, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ECTA, alieleza kuwa hiyo imetokana na mabadiliko ya kimkakati ya kuanzishwa kwa kituo cha kwanza cha kutathmini ubora wa kahawa Afrika Mashariki, shirika la habari la Ethiopia liliripoti.

Mamlaka zinasema kuwa haki za kuuza kahawa nje ya nchi pia zilipewa wakulima waliokuwa na leseni, kuwawezesha zaidi ya 100 miongoni mwao kuuza kahawa nje ya nchi.

Serikali inasema mpango wake wa kuhifadhi mazingira umesaidia kuanzisha masoko mapya 20 ya kuuza kahawa yake, kuondoa utegemezi wa wanunuzi wa kawaida, mamlaka ziliongeza.

Hussein Ambo, Rais wa Chama cha Ushirika cha Kahawa cha Ethiopia, anasema kuna mipango ya pamoja ya kuimarisha soko la kahawa la Ethiopia kupitia juhudi za kitaifa na hafla za kimataifa, ikiwemo Maonesho ya Kitalii ya Kahawa 2025.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us