MICHEZO
1 dk kusoma
Congo-Brazzaville yafanya mabadiliko ya benchi la ufundi kabla ya mashindano ya CHAN
Congo-Brazzaville iko kwenye kundi D, linaloaminika kuwa "kundi la kifo".
Congo-Brazzaville yafanya mabadiliko ya benchi la ufundi kabla ya mashindano ya CHAN
Hivi karibuni Ngatsono alipata leseni ya ukocha ya daraja A la CAF. / CAF
27 Juni 2025

Shirikisho la soka la Congo (FECOFOOT) limemteua Barthélémy Ngatsono kuwa kocha mkuu, hatua muhimu katika kubadilisha benchi la ufundi kwa timu yake ya taifa ya kwanza wakati wakijiandaa kwa mechi za kombe la Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN).

Hatua hii ina maana Ngatsono anarudi kuinoa timu ya taifa.

FECOFOOT inasema ina nia ya kuipa nguvu timu hiyo, wakibakisha tu kocha wa viungo Éric Moukouyou.

Uongozi huo mpya unatarajiwa “kuongeza nguvu na ufundi pamoja na nidhamu” kabla ya mashindano ambayo yatakuwa na wenyeji wenza Kenya, Tanzania na Uganda kutoka Agosti 2 hadi 30.

Congo iko kwenye kundi D, linaloaminika kuwa "kundi la kifo", pamoja na mabingwa wa sasa Senegal, vigogo wa Afrika Magharibi Nigeria, na Sudan.

Ngatsono atasaidiwa katika jukumu hilo na kocha msaidizi Cédric Nanitelamio, ambao wote wamepata leseni ya ukocha ya daraja la A la shirikisho la soka barani Afrika, CAF, taarifa kwenye mtandao wa CAF ilisema.

Kuteuliwa kwao kunafuata mtindo wa mashirikisho ya Afrika kuwapa nafasi makocha wazawa. Wote Ngatsono na Nanitelamio wakiwa wamepitia kwenye mfumo wa kupata leseni ya ukocha wa CAF.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us