MICHEZO
1 dk kusoma
Benfica yaifunga Bayern Munich kufuzu kwa hatua ya mtoano
Timu ya Benfica imeifunga Bayern Munich na kupata nafasi ya kusonga mbele katika Kombe la dunia la klabu katika hatua ya 16 wakiwa washindi wa kundi C.
Benfica yaifunga Bayern Munich kufuzu kwa hatua ya mtoano
Timu ya Bayern Munich. / Reuters
25 Juni 2025

Kwa ushindi huo wa Benfica inamaanisha timu hiyo ya Ureno itacheza dhidi ya Cheslea ambayo imemaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi D.

Bayern ilikuwa tayari imeshafuzu baada ya vijana hao wa Vincent Kompany kuwafunga Boca Juniors ya Argentina siku ya Ijumaa 2-1

Katika kipindi cha pili Bayern walikuwa na makali zaidi wakati mkwaju wa Aleksandar Pavlovic ulipookolewa na Leroy Sane akakosa nafasi mbili za wazi, na hawakupata fursa ya kusawazisha goli hilo la pekee na hivyo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo.

Bayern sasa inaelekea Miami kucheza mechi yake dhidi ya timu ya Brazil Flamengo, huku kukiwa na uwezekano wa kucheza robo fainali na mabingwa wa bara Ulaya Paris Saint-Germain iwapo wote watafuzu.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us