Katika hali ya kawaida, mnyama farasi huhusishwa na ufahari.
Inaaminika kuwa wanyama hawa huwa ni wa waghali, na kwamba si kila mtu anaweza kuwamudu. Wako wanaopenda michezo ya farasi, ikihusishwa na matajiri.
Hata hivyo, nchini Ethiopia, farasi ni wanyama wa kawaida tu.
Inakadiriwa kuwa Ethiopia ina jumla ya farasi milioni 2.8, na kuifanya kuwa moja ya nchi zenye farasi wengi duniani.
Ethiopia ina aina nane ya farasi wanaotambuliwa kama farasi wa Abyssinia. Ni jambo la kawaida kukutana na kundi la farasi barabarani wakitumika katika shughuli mbalimbali.
Wengi wanapatikana sehemu za nyanda za juu za Ethiopia, ambako ukiwa na dola 100 tu, unaweza kummiliki mnyama huyo.
Vile vile, mnyama huyo hutumika na wakulima kwa shughuli zao za kilimo na pia kubeba na kuvuta mizigo kwa kukutumia mikokoteni.
Kama ilivyo kwa punda katika jamii nyengine, Ethiopia farasi anatumika vivyo hivyo.
Wakati mwingine, farasi hutumika kusafirishia watu kwa malipo.
Matumizi ya farasi nchini Ethiopia yalianza karne za kale wakati nchi hiyo ikiongozwa na wafalme.
Wafalme na watu mashuhuri nchini humo waliripotiwa kuwa farasi hodari na wazuri ambao si tu walitumika kama chombo cha usafiri kutoka eneo moja hadi jingine, bali pia katika vitani.
Shughuli za uwindaji
Farasi wa vita walilindwa kwa makini.Watetezi wa haki za wanyama, wana hofu kuhusu hali ya farasi wengi wa kijamii. Utafiti unaonesha kuwa wanakumbana na changamoto za kiafya kutokana na kazi wanazozifanya na mazingira waliyomo.
Pia wana changamoto ya kubebeshwa mizigo mizito kupita kiasi ambayo kwa kawaida sio jukumu lao.
Huko vijijini, kila mwaka huandaliwa matamasha na mashindani maalumu ya farasi, ambapo farasi bora hushindanishwa.
Hata hivyo, ni kawaida kabisa kuwakuta farasi wamesimama kando ya barabara katika mji mkuu wa Addis Ababa na maeneo mengine, wakiwa wapekwe baada ya kutelekezwa na wenyeji wao.
Wanatunzwa na kutumika kwenye michezo ya kifahari.
Hutumika kuonesha fahari ya nchi hasa wakati kukiwa na ugeni mkubwai.Au kama kuna sherehe za kitaifa au za kidini, wao huletwa wakiwa na mapambo yao.
Wataalamu wamekuwa wakisisitiza kuwa ni vyema kwa serikali kuwekeza zaidi katika programu za kuwasaidia wanyama hawa kote nchini kupata lishe na malezi bora na kuwapa thamani zaidi.
Mbali na kutumika tu nchini wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa wakulima wakiwasafirisha kwa nchi nyingine pia.