AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa atoa sababu za 'kumtimua' naibu waziri wa biashara
Andrew Whitfield ni mwanachama wa DA, chama kilichoshiriki kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na chama tawala cha ANC, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2024.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa atoa sababu za 'kumtimua' naibu waziri wa biashara
Whitfield ni mwanachama wa DA, chama ambacho kiliunda serikali ya pamoja na chama cha ANC baada aya uchaguzi mkuu wa 2024 / picha: @andrewhitfield / Public domain
27 Juni 2025

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameweka wazi sababu za kumtimua Andrew Whitfield kutoka nafasi ya Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushindani, uamuzi alioufanya Juni 25, 2025.

“ Si jambo la kawaida kwa rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini kutoa sababu za kuteuliwa au kufukuzwa kazi kwa wajumbe wa serikali,” alisema Rais Ramaphosa kupitia taarifa yake.

Whitfield ni mwanachama wa DA, chama kilichoshiriki kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na chama tawala cha ANC, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2024.

Mwanasiasa huyo, alikuwa sehemu ya wajumbe waliosafiri kwenda nchini Marekani mwezi Februari mwaka kuu, kufuatia kudorora kwa uhusiano kati ya Marekani na Afrika Kusini.

“Lakini kwa sababu ya taarifa kadhaa potofu haswa kutoka kwa kiongozi wa chama cha DA John Steenhuisen na Whitfield mwenyewe, ni muhimu kwangu kutoa taarifa ya umma juu kuhusu kuondolewa kwa Whitfield,” alisema Rais Ramaphosa.

“ Whitfield aliondolewa kama Naibu Waziri kwa sababu alifanya ziara ya kimataifa bila idhini ya rais. Safari yake ya kwenda Marekani ilikiuka wazi sheria za udhibiti wa mwenendo wa wajumbe,” aliongeza.

Kulingana na kiongozi huyo wa Afrika Kusini, ni lazima safari zote za kimataifa za wajumbe zifuate idhini ya rais, akimkosoa Whitfield kwa kutofuata utaratibu huo.

Hata hivyo, katika mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni nchini humo, Whitfield amesema kuwa hakuna maelezo yoyote aliyopokea kuhusu kufukuzwa kwake.

Mwanasiasa huyo alisisitiza kuwa, alikuwa ameomba ruhusa ya kusafiri kwenda Marekani kutoka kwa rais mwenyewe, bila kupata majibu yoyote, japo aliomba msamaha hapo baadaye.

Bw Whitfield aliondolewa kama Naibu Waziri kwa sababu alifanya ziara ya kimataifa bila idhini ya Rais. Safari yake ya kwenda Marekani ilikuwa ukiukaji wa wazi wa sheria na mazoea yaliyowekwa ya kudhibiti mwenendo wa Wajumbe wa Mtendaji. Sharti hili linajulikana kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wote.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us