MICHEZO
2 dk kusoma
Khaman Maluach wa Sudan Kusini ajiunga na ligi ya NBA
Khaman Maluach amepata nafasi katika ligi ya mpira wa kikapu ya NBA licha ya viza yake kubatilishwa na serikali ya Trump.
Khaman Maluach wa Sudan Kusini ajiunga na ligi ya NBA
Khaman Maluach wa Sudan Kusini. / Reuters
26 Juni 2025

Siku ya Jumatano, 25 Juni, mchezaji huyo alichaguliwa kuwa mchezaji wa Phoenix Suns. Suns walimchagua kama mchezaji wa kumi baada ya Houston Rockets kuchukuwa nafasi hiyo katika raundi ya kwanza.

Ana urefu wa futi 7 na inchi 7 na anasemekana kuwa na uwezo wa kukabiliana na wachezaji wa timu pinzani. Maluach ana umri wa miaka 18, na pia ana uwezo mzuri wa kuwa mchezaji wa kulipwa wa safu ya ulinzi.

Mwezi Aprili, Rais Donald Trump na serikali yake alitangaza kuwa raia wa Sudan Kusini wenye viza za Marekani vibali vyao vitabatilishwa "mara moja.”

"Nachukua hatua ya kubatilisha vibali vyote vya wale wenye pasi za kusafiri za Sudan Kusini na kuweka marufuku ya kuingia Marekani, mara moja, kutokana na serikali ya mpito ya Sudan Kusini kukataa kurudishwa kwa raia wao kwa muda ufaao,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio aliandika katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii Aprili 5.

Khaman Maluach alizaliwa katika eneo la Rumbek, Sudan Kusini na akiwa mdogo wakaishi nchini Uganda kama wakimbizi yeye pamoja na wazazi wake na ndugu zake.

Waendesha boda boda ndiyo walimhamasisha kucheza mpira wa kikapu kulingana na urefu wake. Baadaye alijiunga na kituo cha NBA barani Afrika, Saly nchini Senegal ambapo wanafunzi wanapata fursa ya kucheza mpira wa kikapu na kuendelea na masomo pia.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us