MICHEZO
1 dk kusoma
Mkenya John Korir ashinda mbio za Boston, Mtanzania ni wa pili
Kwa ushindi huu wa Jumatatu, Korir amefanya kama alivyofanya kaka yake, Wesley Korir, aliyeshinda marathon ya Boston mwaka 2012.
Mkenya John Korir ashinda mbio za Boston, Mtanzania ni wa pili
Mkenya John Korir ameshinda mbio za Boston Marathon Jumatatu akimaliza katika muda wa saa 2, dakika 4 na sekunde 45. / Reuters
21 Aprili 2025

Mkenya John Korir alijitahidi kukabiliana na mwanzo mbaya na kumaliza mshindi wa mbio za marathon za Boston Jumatatu, akimaliza katika muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 45.

Mshindi huyu wa marathon ya Chicago mwaka 2024 alikabiliana na hali hiyo vizuri na kuwaacha nyuma wanariadha wengine, kabla ya kumaliza mbio hizo akiwa kidedea.

Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu alimaliza wa pili katika muda wa 2:05:04, akipambana na Mkenya mwingine hadi mwisho ambapo Cybrian Kotut alikuwa wa tatu kumaliza mbio hizo.

Sisay Lemma wa Ethiopia alishinda mbio hizo za Boston mwaka 2024, akimaliza katika muda wa saa 2, na dakika 6.

Kwa ushindi huu wa Jumatatu, Korir amefanya kama alivyofanya kaka yake, Wesley Korir, aliyeshinda mbio za marathon za Boston mwaka 2012.

Kwa upande wa wanawake Mkenya Sharon Lokedi alishinda katika muda wa saa mbili, dakika 17 na sekunde ishirini na mbili. Mkenya mwingine Hellen Obiri alikuwa wa pili na mwanariadha wa Ethiopia Yalemzerf Yehualaw akamaliza wa tatu.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us