Maandamano nchini Kenya yaliongozwa na vijana maarufu Gen Z ambao hawakuwa na kiongozi, ila waliwasiliana kwa njia ya mitandao.
Maandamano yalifanyika katika mji mkuu wa Nairobi na kaunti nyengine, vijana wakipinga Muswada wa Fedha 2024 na kutaka utupiliwe mbali.
Polisi walijitokeza kujaribu kuwa kinga waandamanaji.
Vijana hawakutishiwa na vitoa machozi ambavyo polisi walitumia kujaribu kuwatawanya.
Waandamanani walishinda wakisisitiza kuwa wanatoa hoja zao kwa amani.
Maandamano yalifanyika kwa siku kadhaa huku vijana wakiongezeka kila siku.
Wengine walionyesha ujasiri wao licha ya polisi kutumia vitoa machozi.
Baadhi ya waandamanaji walikamatwa na polisi na wengine waliripotiwa kupigwa risasi. Kwa jumla vijana 60 waliripotiwa kufa kwa maandamano ya Juni 2024.
Vijana hawakuwaogopa polisi huku wengine wakiwakaribia na kuwaomba wasiwapige risasi.
Mwamko wa Genz nchini Kenya ulifungua wimbi jipya la wananchi kuamka na kujitetea moja kwa moja dhidi ya serikali na si kiutegemea mashirika au vikundi vya watetezi wa haki.