ULIMWENGU
1 dk kusoma
Papa Francis aadhimisha miaka 12 ya upapa akiwa hospitalini
Vatican inasema papa Francis alionja keki ya kusherehekea miaka 12 ya upapa, aliomba na kufanya mazoezi yake ya kupumua
Papa Francis aadhimisha miaka 12 ya upapa akiwa hospitalini
Papa Francis alitawazwa kama Papa Machi 2013 / AA
14 Machi 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amekuwa na "usiku mwingine mtulivu" katika hospitali ya Roma ambapo amekuwa akiugua nimonia katika mapafu yote kwa mwezi mmoja, Vatican ilisema Ijumaa.

Ingawa hayuko tena katika hali mbaya, papa huyo mwenye umri wa miaka 88 bado anapokea usaidizi wa kupumua kupitia mrija wa pua wakati wa mchana na oksijeni wakati wa usiku.

Vatican ilisema Papa Francis alifanyiwa matibabu ya viungo Alhamisi na vile vile anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Gemelli.

Pia alionja keki ya kusherehekea miaka 12 ya upapa, aliomba na kufanya mazoezi yake ya kupumua.

Ofisi ya mawasiliano ya Vatican ilisema itatoa taarifa nyingine kuhusu maendeleo ya hali yake ya afya Ijumaa jioni, lakini inaweza kuacha kutuma taarifa ya kila siku asubuhi.

Mazungumzo sasa yanageukia kuhusu wakati gani anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Lakini kukaa kwake hospitalini ambako kulianza Februari 14, kumezua shaka kuhusu uwezo wake wa kuongoza takriban Wakatoliki bilioni 1.4 duniani.

"Inachukua muda kwa mwili wa umri wa miaka 88 ulioathiriwa na nimonia kupona, pia katika suala la nishati, nguvu," ofisi ya Vatican ilisema.


CHANZO:REUTERS
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us