Hawa ndiyo makardinali Waafrika watakaoshiriki kumchagua Papa mpya
AFRIKA
3 dk kusoma
Hawa ndiyo makardinali Waafrika watakaoshiriki kumchagua Papa mpyaKati ya makadinali 250, ni 135 pekee watakaomchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani, kufuatia kifo cha Papa Francis kilichotokea Aprili 21, 2025. Kati ya hao, 18 wanatoka Afrika.
Papa huchaguliwa na makardinali zaidi ya mia katika kongamano la siri huko Vatican / TRT Afrika Swahili
22 Aprili 2025

Mchakato wa kumtafuta mrithi wa Papa Francis unategemewa kuanza kulingana na taratibu za Kanisa Katoliki, kufuatia kifo cha kiongozi huyo siku ya Aprili 21, 2025. Makardinali wapatao 135, wanatarajiwa kukutana Vatican kuanza mchakato huo wa siri wa kumpata Papa mpya.

Kati ya makadinali 252 ambao wako duniani, ni 135 pekee watakaoshiriki katika ‘mjumuiko wa kumtafuta Papa’ au ‘Papal enclave‘, kama inavyofahamika, kulingana na nafasi na hadhi zao. 

Kwa taratibu na sheria za Kanisa Katoliki, maarufu kama ‘Canon Law’, makardinali hao wanapaswa kuwa na chini ya miaka 80, yaani wawe wamezaliwa baada ya Aprili 1945, pamoja na vigezo vingine kama kuwa na afya nzuri na ushawishi. 

Kati ya makadinali 135 wenye uwezo wa kupiga kura, 18 wanatokea bara la Afrika na wanatarajiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa kihistoria.

Ifuatayo ni orodha ya makardinali waafrika wanaotarajiwa kuwa sehemu ya jumuiko hili, kulingana na orodha zilizotolewa na vyanzo tofauti na hata baadhi yao wakipigiwa upatu kurithi cheo hicho:

  • Jean-Paul Vesco OP - Algeria : Alizaliwa Machi 10, 1962, ni Askofu Mkuu wa Alger

  • Philippe Ouédraogo - Burkina Faso: Alizaliwa Disemba 31, 1945 ni ni Askofu Mkuu mstaafu wa Ouagadougou

  • Dieudonné Nzapalainga CSSp - Jamhuri ya Afrika ya Kati: Alizaliwa Machi 14, 1967, ni Askofu Mkuu wa Bangui

  • Fridolin Ambongo Besungu OFMCap - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo: Alizaliwa Januari 24, 1960, ni Askofu wa Kinshasa

  • Berhaneyesus Demerew Souraphiel CM - Ethiopia: Alizaliwa Julai 14, 1948, ni Askofu Mkuu wa Addis Ababa

  • Peter Turkson - Ghana: Alizaliwa Oktoba 11, 1948, ni Askofu Mkuu mstaafu wa Cape Coast

  • Robert Sarah - Guinea: Alizaliwa Juni 15, 1945, ni Askofu Mkuu mstaafu wa Conakry

  • Jean-Pierre Kutwa - Cote d’Iviore: Alizaliwa Disemba 22, 1945,ni Askofu Mkuu wa Abidjan

  • Ignace Bessi Dogbo - Cote d’Iviore: Alizaliwa Agosti 17, 1961, ni Askofu wa Abdijan

  • John Njue - Kenya: Alizaliwa Januari 1, 946, ni Askofu Mkuu mstaafu wa Nairobi

  • Désiré Tsarahazana - Madagascar: Alizaliwa Juni 13, 1954, ni Askofu Mkuu wa Toamasina

  • Cristóbal López Romero SDB - Morocco: Alizaliwa Mei 19, 1952, ni Askofu Mkuu wa Rabat

  • Peter Okpaleke - Nigeria: Alizaliwa Machi 1, 963, ni Askofu wa Ekwulobia

  • Stephen Brislin - Afrika Kusini: Alizaliwa Septemba 24, 1956, ni Askofu Mkuu wa Cape Town, Kaapstad

  • Stephen Ameyu Martin Mulla - Sudan Kusini: Alizaliwa Januari 10, 1964, ni Askofu Mkuu wa Juba

  • Protase Rugambwa - Tanzania: Alizaliwa Mei 31, 1960, , ni Askofu Mkuu wa Tabora

  • Antoine Kambanda - Rwanda: Alizaliwa Novemba 10, 1958, ni Askofu Mkuu wa Kigali

  • Arlindo Gomes Furtado - Cape Verde: Alizaliwa Novemba 15, 1949, ni Askofu wa Santiago de Cabo Verde

Ushiriki wa makardinali hawa unaashiria nafasi na ushawishi wa Afrika katika Kanisa Katoliki, na pia kuimarisha mchango wa bara hilo katika masuala ya kiimani na kijamii duniani.

Papa Francis alikuwa Papa wa kwanza kutoka nje ya Ulaya na huenda utamaduni huu ukaendelezwa kwa kumchagua papa kutoka Afrika, tukio ambalo litatilia mkazo uzito wa imani ya kikatoliki katika bara lililo na wakatoliki zaidi ya milioni 265 ambayo ni asilimia 19 ya wakatoliki duniani.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us