Tanzania na maajabu ya mchanga unaohama ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
Tanzania na maajabu ya mchanga unaohama ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
Japo si rahisi kuona kwa macho namna mchanga huo unavyohama, lakini unaweza kubahatisha kuona jinsi unavyotiririka.
3 Julai 2025

Ukipanga safari ya kwenda Tanzania, basi usitarajie kuona wanyama pori tu.

Ukipata nafasi, basi fika eneo la mashariki la uwanda wa hifadhi ya taifa ya Serengeti, karibu na Olduvai Gorge ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Ni katika eneo hilo, ambako utastajabu kuona maajabu ya matuta makubwa ya mchanga unaohama.

Mchanga huu huhama kwa mita 15 hadi 29 kwa mwaka bila kubadili umbo lake la mwezi mchanga ukiwa umejikusanya pamoja bila kuacha mabaki nyuma.

Mchanga huo hupeperushwa na mawimbi ya upepo kuelekea eneo la magharibi hadi kuvuka eneo la tambarare.

Tukio hili ni mojawapo ya mambo ya kuvutia na kukuacha kinywa wazi uwapo ndani na eneo la Ngorongoro nchini Tanzania.

Kuhama hama huku kumesafisha sehemu nyepesi za majivu kutoka eneo hilo, na kuacha nyuma madini ya chuma yenye rangi nyeusi ambayo yaliunda mchanga huo.

Ukilinganisha na mchanga wa eneo, rangi ya mchanga uhamao ni mweusi


Tuta la mchanga hufikia urefu wa mita tisa na kunyoosha urefu wa mita 100 kwenye mikondo yake.

Unaweza usihisi kuwa mchanga huo hauendi sehemu yoyote, kwani huhama kwa njia ya mtiririko.

Utagundua uhamaji wake kutokana na alama za mawe zilizowekwa eneo hilo, zikionesha mahali mchanga ulipo kwa wakati huo, na wapi ulikuwepo hapo kabla.

Michanga hiyo hujumuisha majivu ya volkeno, yenye nguvu ya sumaku, yenye uwezo wa kushikilia chembechembe za mchanga pamoja.

Wageni wanaofika eneo hili, hustaajabu sumaku ya mchanga huu ukinatisha simu zao za mikononi, na hata vitu vingine vyenye asili ya chuma.


Kwa mfano hata ukitupa mchanga hii hewani utagundua jinsi unavyoungana tena ikirejea ardhini.

Wanasayansi wanaamini matuta hayo ya mchanga yaliundwa zaidi ya miaka milioni 3 iliyopita kutokana na mlipuko mkubwa wa volkano hai ya mlima wa Oldonyo Lengai, ulioko mita 60 Kaskazini Mashariki mwa eneo hilo.

Matuta ya machanga yamehamahama na kubadilisha umbo na hata mweleko wale.
Hata hivyo jamii ya Maasai wanaamini Mlima Oldonyo Lengai, au Mlima wa Mungu kama wauitavyo, ndiyo chanzo kikubwa cha matuta ya mchanga uhamao.

Hivyo, huonesha heshima kwa matuta haya na hukusanyika hapa, hasa nyakati za ukame mkali na kutoa kafara za mbuzi ili kufurahisha miungu kwa ajili ya kupata mvua.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us