Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ametoa rai kwa jumuiya wa Kikristo duniani kuonesha msimamo ili kusaidia kumaliza janga la kibinadamu huko Gaza, huku akipongeza msimamo wa Vatican wa kuunga mkono uwepo wa dola mbili katika kumaliza mgogoro kati ya Israel na Palestina.
"Nimefurahi kukutana Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani na kiongozi wa dola ya Vatican, wakati wa ziara yangu nchini humo kwa ajili kushiriki programu ya ‘Undugu Kiuchumi: Maadili na Utofauti', iliyoandaliwa Vatican,” alisema Erdogan katika taarifa yake kwenye mitandao ya jamii siku ya Jumatano.
"Majadiliano yetu yaliangazia matatizo yanayoendelea Gaza," alisema. "Tulibadilishana mawazo kuhusiana na mambo muhimu kuhusu jumuiya ya Wakristo duniani kuonesha msimamo wa kumaliza machafuko na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia."
Aliongeza Mke wa Rais wa Uturuki: "Nilifarijika na namna Vatican inayounga mkono suala la uanzishwaji wa dola mbili kama suluhisho la kudumu la upatikanaji amani ya Palestina."
Wawili hao, pia walizungumzia masuala ya mazingira, ikiwemo mkakati wa “Kutokewepo na Taka".
"Tulikubaliana kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni janga lenye kuathiri binadamu wote bila kujali eneo walipo," alisema. "Kwa muktadha huu, nilionesha haja ya ushirikiano kati ya Uturuki na Vatican katika kupambana na janga hilo. Tulifanya tathmini ya maeneo ya kushirikiana."