2 Julai 2025
Jeshi la polisi nchini Zambia linawashikilia raia 4 wa China baada ya kula njama za kuiba shehena na madini ya zinki yenye thamani ya zaidi ya dola 45,000.
Shehena hiyo ya madini ilikuwa inatokea mgodi wa STL nchini DRC, ikisafirishwa kuelekea Singapore, kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la polisi la Zambia, Rae Hamoonga.
Kwa mujibu wa Hamoonga, shehena hiyo ilikuwa itoke eneo hilo kupitia njia ya Dar es Salaam, kabla ya kuzuiliwa ikiwa kwenye lori lenye namba za usajili wa Tanzania.
“Kwa sasa, watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi huku lori hilo likishikiliwa kama kaka kidhibiti cha ushahidi,” alieleza, akiongeza kuwa vyombo vya usalama vinaendelea na mapambano wizi wenye kuvuka mipaka.